MASOMO
YA MISA, JANUARY 4, 2021
JUMATATU
BAADA YA EPIFANIA
SOMO
1
1Yoh.
3:22-4:6
Wapenzi:
Lolote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda
yapendezayo machoni pake. Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la
Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri. Naye
azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye, naye ndani yake, kwa huyo Roho
aliyetupa.
Wapenzi,
masiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa
sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa
Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na
Mungu. Na kil aroho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya
mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Ninyi,
watoto wadogo, mwatokana na Mungu; nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye
ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Hao ni wa dunia; kwa hiyo
wanena ya dunia na dunia huwasikia. Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu
atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa
kweli, na roho ya upotevu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
2:7-8, 10-11 (K) 8a
(K)
Nitakupa mataifa kuwa urithi wako.
Nitaihubiri
amri; Bwana aliniambia,
Ndiwe
mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
Uniombe,
nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,
Na
miisho ya dunia kuwa milki yako. (K)
Na
sasa, enyi wafalme, fanyeni akili,
Enyi
waamuzi wa dunia, mwadibiwe.
Mtumikieni
Bwana kwa kicho;
Shangilieni
kw akutetemeka. (K)
SHANGILIO
Mt.
4:16
Aleluya,
aleluya.
Watu
wale waliokaa katika giza wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na
uvuli wa mauti mwanga umewazukia.
Aleluya.
INJILI
Mt.
4:12-17, 23-25
Siku
ile, Yesu aliposikia ya kwamba Yohane amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;
akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa
Zabuloni na Naftali: ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi
ya Zabuloni nan chi ya Naftali, Njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya
mataifa, Watu wale waliokaa katika giza. Wameona mwanga mkuu, nao waliokaa
katika nchi na uvuli wa mauti mwanga umewazukia. Tokea wakati huo Yesu alianza
kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Naye
alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na
kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna
katika watu. Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote
waliokuwa hawawezi, walioshikw ana maradhi mbalimbali na mteso, wenye pepo, na
wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya. Na makutano mengi wakamfuata,
kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furahaya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment