MASOMO
YA MISA, JANUARI 9, 2021
JUMAMOSI
BAADA YA EPIFANIA
SOMO
1
1Yoh.
5:14-21
Wapenzi:
Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi
yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba
tunazo zile haja tulizomwomba. Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya
mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya
mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.
Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
Twajua
ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na
Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; bali
yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. Twajua ya kuwa
sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. Nasi twajua kwamba
Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa
kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake
Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. Watoto wadogo,
jilindeni nafsi zenu na sanamu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
149:1-6, 9 (K) 4
(K)
Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake.
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Sifa
zake katika kusanyiko la watauwa.
Israeli
na amfurahie Yeye aliyemfanya,
Wana
wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao. (K)
Na
walisifu jina lake kwa kucheza,
Kwa
matari na kinubi wamwibie.
Kwa
kuwa Bwana awaridhia watu wake,
Huwapamba
wenye upole kwa wokovu. (K)
Watauwa
na waushangilie utukufu,
Waimbe
kwa sauti kuu vitandani mwao.
Sifa
kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,
Hiyo
ndiyo heshima ya watauwa wake wote. (K)
SHANGILIO
Lk.
7:16
Aleluya,
aleluya,
Nabii
mkuu ametokea kwetu; Na mungu amewaangalia watu wote.
Aleluya.
INJILI
Yn.
3:22-30
Siku
ile, Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko
pamoja nao, akabatiza. Yohane naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na
Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea wakabatizwa.
Maana Yohane alikuwa hajatiwa gerezani.
Basi
palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohane na Myahudi mmoja juu ya utakaso.
Wakamwendea Yohane, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya
Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea.
Yohane
akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lolote isipokuwa amepewa kutoka
mbinguni. Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo,
bali nimetumwa mbele yake. Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini
rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, alifurahia sana sauti
yake bwana arusi. Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali
mimi kupungua.
Neno
la Bwana… Sifa kwako
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment