MASOMO YA MISA, JANUARI 6, 2021
JUMATANO
BAADA YA EPIFANIA
SOMO
1
1Yon.
4:11-18
Wapenzi,
ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu
aliyemwona Mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, nap endo
lake limekamilika ndani yetu. Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani
yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. Na sisi tumeona na
kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Kila akiriye
ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.
Nasi
tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo,
naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya
hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.
Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lilio kamili huitupa nje hofu, kwa maana
hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
72:1-2,10,12-13 (K) 11
(K)
Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Ee
Mungu, mpe mfalme hukumu zako.
Na
mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua
watu wako kwa haki,
Na
watu wako walioonewa kwa hukumu. (K)
Siku
zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,
Na
wingi wa Amani hata mwezi utakapokoma
Na
awe na enzi toka bahari hata bahari,
Toka
mto hata miisho ya dunia. (K)
Wafalme
wa Tarshisi na visiwa walete kodi,
Wafalme
wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
Naam,
wafalme wote na wamsujudie;
Na
mataifa yote wamtumikie. (K)
Kwa
maana atamwokoa mhitaji aliapo,
Na
mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi
Atamhurumia
aliye dhaifu na maskini,
Na
nafsi za wahitaji ataziokoa. (K)
SHANGILIO
Lk.
4:18-19
Aleluya,
aleluya,
Bwana
amenituma kuwahubiri maskini habari njema, na kuwatangazia wafungwa kufunguliwa
kwao.
Aleluya.
INJILI
Mk.
6:45-52
Baada
ya watu elfu tano kula na kushiba, mara Yesu aliwalazimisha wanafunzi wake
wapande mashuani, watangulie kwenda ng’ambo hata Bethsaidia, wakati yeye
alipokuwa akiwaaga mkutano. Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani
kuomba.
Na
kulipokuwa jioni mashua ilikuwa katikati ya bahari, na yeye yupo peke yake
katika nchi kavu. Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo
ulikuwa wa mbisho; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea,
akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita. Nao walipomwona anatembea juu ya
bahari, walidhani ya kuwa ni kivuli, wakapiga yowe, kwa kuwa wote walimwona,
wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.
Akapanda mle chomboni walimo; upepo ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao; kwa
maana hawakufahamu habari za ile mikate, lakini mioy yao ilikuwa mizito.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
No comments:
Post a Comment