MASOMO
YA MISA, JANUARI 30, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 3 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
11:1 – 2, 8 – 19
Imani
ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.
Kwa
Imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopata kuwa
urithi; akatoka asijue aendako. Kwa Imani alikaa nchi isiyo yake, akikaa katika
hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana
alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni
Mungu.
Kwa
Imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita
wakati wake, kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Na kwa ajili
ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota
za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.
Hawa
wote wakafa katika Imani, wasijazipokea zile ahadi bali wakaziona tokea mbali
na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao
wenyewe. Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipa nafsi ya
kurejea. Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo
Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.
Kwa
Imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea
hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanwe, mzaliwa pekee; Naam, yeye aliyeambiwa,
Katika Isaka uzao wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata
kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Lk.
1:69 – 75 (K) 68
(K)
Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake.
Ametusimamishia
pembe ya wokovu
Katika
mlango wa Daudi mtumishi wake.
Kama
alivyosema tangu mwanzo
Kwa
kinywa cha manabii wake watakatifu. (K)
Tuokolewe
na adui zetu
Na
mikononi mwao wote wanaotuchukia:
Ili
kuwatendea rehema baba zetu,
Na
kulikumbuka agano lake takatifu. (K)
Uapo
aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,
Ya
kwamba atatujalia sisi,
Tuokoke
mikononi mwa adui zetu,
Na
kumwabudu pasipo hofu
Kwa
utakatifu na kwa haki
Mbele
zake siku zetu zote. (K)
SHANGILIO
Yn.
14:23
Aleluya,
aleluya,
Mtu
akinipenda, atalishika neno langu, na baba yangu atampenda, na sisi tutakuja
kwake.
Aleluya.
INJILI
Mk.
4:35-41
Siku
ile kulipokuwa jioni, Yesu akawambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo. Wakauacha
mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine
vilikuwako pamoja naye. Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga
chombo hata kikaanza kujaa maji. Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala
juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma,
kukawa shwari kuu. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna Imani bado?
Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari
humtii?
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment