“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumamosi,
Januari 30, 2021,
Juma
la 3 la Mwaka wa Kanisa
Ebr
11:1-2, 8-19;
Lk
1: 69-75;
Mk
4: 35-41
KUMWAMINI
YESU KWA MAISHA YETU!
Bahari
na mawimba yana mtii Mungu kwasababu ni sehemu ya uumbaji wake. Na wala hakuna
tatizo kubwa sana kwa Mungu ambalo anashindwa kulitatua. Hofu zetu hazina
mwisho, matatizo yetu yanatusumbua, kwasababu sisi wenyewe tumechagua
kuyakabili wenyewe kwa nguvu zetu. Wafuasi walikuwa ni watu wa kawaida kama
sisi. Hata wakiwa kati ya Yesu wana ogopeshwa na gharika! Laiti kama Mwanadamu
angelijua kukabidhi hofu zake na maumivu yake kwa Mungu!
Ni
rahisi sana kukata tamaa katika maisha. Ni rahisi zaidi kuelekeza mwelekeo wote
kwenye matatizo na kuacha mengine yanayo tuzunguka. Hata kama ingekuwa ni
maneno ya hasira na ya kuumiza kutoka kwa wengine, matatizo ya kifamilia,
matatizo ya umma, ukosefu wa fedha nk. Kuna kila sababu ya kila mmoja wetu
kuanguka kwenye mtego wa hofu, kuchanganyikiwa, kuumia na kuwa na shauku. Lakini
ilikuwa ni kwasababu ya sababu hizi Yesu aliruhusu tukio hili litokee akiwa na
wafuasi wake. Alikuwa kwenye boti na wafuasi wake akaruhusu wafuasi wakumbwe na
gharika kuu, wakati yeye akiwa amelala, ili aweze kuleta ujumbe wa kufaa kwetu
sisi wote.
Katika
habari hii, wafuasi walilenga kwenye kitu kimoja tuu: walikuwa waangamie!
Bahari ilikuwa ikiwasukasuka na waliogopa maangamizi makubwa! Lakini kwa
kupitia yote hayo, Yesu alikuwa pale akionekana amelala, akiwasubiri waweze
kumwamsha. Na walipo mwamsha, alikemea gharika na hali ikawa shwari. Hili ni
kweli pia katika maisha yetu. Sisi mara nyingi tunaruhusu matatizo mengi
tunayopata yatutese na kutusukasuka. Ufunguo ni kwamba tunapaswa kugeuza macho
yetu na kumwelekea Yesu. Muone mbele yako amelala, anakusubiri umwamshe. Yupo
daima, akikusubiri na yupo tayari daima. Kumwamsha Bwana wetu ni rahisi kama
ilivyo rahisi kugeuza macho yetu kutoka katika gharika na kusadiki uwezo wake
wa Kimungu. Yote ni kuwa na Imani kwake tu. Imani kamili. Je, una mwamini yeye?
Tumwache Yesu achukue nafasi ya kila kitu katika maisha yetu tuliopo.
Anatupenda na kweli atatujali wote.
Sala:
Bwana, ninakugeukia katikati ya changamoto za maisha na ninatamani kukuamsha
uje katika maisha na kunisaidia. Ninatambua upo daima karibu yangu, ukinisubiri
mimi nikuamini wewe kwa kila kitu. Nisaidie nielekeze macho yangu kwako na kuwa
na Imani kamili katika mapendo yako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment