MASOMO
YA MISA, JANUARI 29, 2021
IJUMAA,
JUMA LA 3 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
10:32 – 39
Zikumbukeni
siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano
makubwa ya maumivu; pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi
mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo. Maana mliwaonea huruma wale
waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu,
mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. Basi msiutupe
ujasiri wetu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba
mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo
kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu
ataishi kwa Imani; naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi
hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na
Imani ya kutuokoa roho zetu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
37:3 – 6, 23 – 24, 39 – 40 (K) 39
(K)
Wokovu wa wenye haki una Bwana.
Umtumaini
Bwana ukatende mema,
Ukae
katika nchi upendezwe na uaminifu.
Nawe
utajifurahisha kwa Bwana,
Naye
atakupa haja za moyo wako. (K)
Umkabidhi
Bwana njia yako pia umtumaini
Naye
atafanya;
Ataitokeza
haki yako kama nuru,
Na
hukumu yako kama adhuhuri. (K)
Hatua
za mtu zaimarishwa na Bwana,
Naye
aipenda njia yake.
Ajapojikwaa
hataanguka chini,
Bwana
humshika mkono na kumtegemeza. (K)
Wokovu
wa wenye haki una Bwana,
Yeye
ni ngome yao wakati wa taabu.
Naye
Bwana huwasaidia na kuwaopoa,
Huwaopoa
na wasio haki na kuwaokoa,
Kwa
kuwa wamemtumaini Yeye. (K)
SHANGILIO
1Thes.
2:13
Aleluya,
aleluya,
Lipokeeni
neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya.
INJILI
Mk.
4:26-34
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga
mbegu juu ya nchi; akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu
ikamea na kukua, asivyojua yeye. Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena
suke, kisha ngano pevu katika suke. Hata matunda yakiiva, mara aupeleka mundu,
kwa kuwa mavuno yamefika.
Akasema,
Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani? Ni kama
punje ya haradali, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu
zote zilizo katika nchi, lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti
yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini
ya uvuli wake.
Kwa
mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza
kulisikia; wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake
mwenyewe mambo yote kwa faragha.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment