MASOMO
YA MISA JANUARI 25, 2019
JUMATATU,
JUMA LA 3LA MWAKA
SIKUKUU
YA KUONGOKA KWA MT. PAULO, MTUME
SOMO
1
Mdo
22:3-16
Paulo
aliwaambia makutano, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia,
ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya
baba zetu kwa usahihi nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo
leo hivi; nikawaudhi watu wa njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani
wanaume na wanawake. Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza
wote pia, ambao nalipokea barua kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski,
ili niwalete wale waliokuwa huko hata Yerusalemu, hali wamefungwa, ili
waadhibiwe.
Ikawa
nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru
kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote. Nikaanguka nchi, nikasikia sauti
ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi? Nikajibu, Wewe u nani, Bwana?
Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. Na wale waliokuwa
pamoja nami, waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya Bwana? Bwana
akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote
yaliyoamriwa uyafanye. Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fahari ya nuru ile,
nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikaingia Dameski.
Basi
mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi
wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami akaniambia, Ndugu yangu
Sauli, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile. Akasema, Mungu wa baba zetu
amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na
kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake. Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa
watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. Basi sasa unakawilia nini?
Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Bwana.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
117:1-2 (K) Mk. 16:15
(K)
Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aleluya!
Enyi
mataifa yote, msifuni Bwana,
enyi
watu wote, mhimidini. (K)
Maana
fadhili zake kwetu sisi ni kuu,
na
uaminifu wa Bwana ni wa milele. (K)
SHANGILIO
Yn.
15:16
Aleluya,
aleluya,
Niliwachagua
ninyi, nikawaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kuzaa.
Aleluya.
INJILI
Mk.
16:15-18
Yesu
alionekana na wale kumi na mmoja, akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini,
atahukumiwa. Maana ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu
watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha
kufisha hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata
afya.
Neno
la Bwana… Sifa kwako ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment