“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu
, Januari 25, 2021,
Juma
la 3 la Mwaka wa Kanisa
Sikukuu
ya kuongoka kwa Mt. Paulo, Mtume
Mdo
22: 3-16;
Zab
117: 1-2 (R.) Mk 16:15
Mk
16: 15-18.
KUKUTANA
NA YESU!
Habari
ya Paulo ni kuhusu yeye kukutana na Yesu. Baada ya kukutana na Yesu, hakuhitaji
kitu kingine zaidi. Hakuna kazi iliokuwa ngumu sana wala jaribuu kubwa sana la
kumshinda. Injili ya leo imetoka katika sehemu ya mwisho ya Injili ya Marko. Na
inaeleza kuhusu maelekezo anayo wapa Yesu wafuasi wake kabla hajaondoka kwa
mara ya mwisho. Ni maneno yanayo ingia sana kwa Paulo. Yanaanza na maelekezo ya
kutangaza habari njema kwa kila kiumbe. Hili ndilo alilokuwa akilifanya Paulo
baada ya kufika kwa watu wa mataifa, kupita kote huko ambako kwa sasa kunaitwa,
Uturuki, kupitia Ugiriki na makedonia na mpaka Roma. “Watakao amini na
kubatizwa wataokolewa”. Paulo aliishi vyema mpaka akifikia kusema “sio mimi
naishi bali ni Kristo anaishi ndani mwangu”. Alama ya muunganiko kamili na
Bwana.
Kuongoka
sio kitu kinacho tokea mara moja katika maisha. Ni kitu ambacho kinatokea kwetu
mara nyingi katika maisha yetu. Tuwe tayari kujibu kila wakati Bwana wetu
anapotuita kwa kitu kikubwa zaidi. Tunaitwa kufungua macho ya mioyo yetu.
Tunaitwa kutambua upofu wetu kwenye wito wa Yesu, na kujiandaa kwa toba ya
kweli. Kwani Yesu anataka kututuma kila mmoja wetu Ulimwenguni kote kuhubiri
habari njema ya msamaha na kuendeleza kazi ambayo yeye ameianzisha ulimwenguni.
Sala:
Bwana, ninaomba nikubali kama Paulo, wito wako wa kukutana na wewe. Ninaomba
nikaribishe wito wako kwa moyo wazi. Ninaomba niendelee kutembea katika njia za
wito wako siku zote za maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment