MASOMO
YA MISA, JANUARI 14, 2021
ALHAMISI,
JUMA LA 1 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
3:7 – 14
Roho
Mtakatifu asema: Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu,
kama wakati wa kukasirisha, siku ya kujaribiwa katika jangwa, hapo baba zenu
waliponijaribu, wakanipima, wakaona matendo yangu miaka arobaini. Kwa hiyo
nalichukizwa na kizazi hiki, nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa;
hawakuzijua njia zangu; kama nilivyoapa kwa hasira yangu, hawataingia rahani
mwangu. Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa
kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. Lakini mwonyane kila siku,
maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa
uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
95:6 – 11 (K) 8
(K)
Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu.
Njoni,
tuabudu, tusujudu,
Tupige
magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa
maana ndiye Mungu wetu,
Na
sisi tu watu wa malisho yake,
Na
kondoo za mkono wake. (K)
Ingekuwa
heri leo msikie sauti yake!
Msifanye
migumu mioyo yenu,
Kama
vile huko Meriba, kama siku ya Masa jangwani.
Hapo
waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima
wakayaona matendo yangu. (K)
Miaka
arobaini nalihuzunika na kizazi kile,
Nikasema,
Hao ni watu waliopotoka mioyo,
Hawakuzijua
njia zangu.
Nikaapa
kwa hasira yangu
Wasiingie
rahani mwangu. (K)
SHANGILIO
Mt.
11:25
Aleluya,
aleluya,
Nakushukuru,
Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na
akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.
INJILI
Mk.
1:40-45
Siku
ile mtu mwenye ukoma akaja kwa Yesu, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia,
Ukitaka, waweza kunitakasa. Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa,
akamwambia, Nataka, takasika. Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.
Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara, akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno
lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa
kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.
Lakini
akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu
asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwako nje mahali pasipokuwa na
watu, wakamwendea kutoka kila mahali.
Neno
la Bwana… Sifa kwako ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment