MASOMO
YA MISA, JANUARI 10, 2021
SIKUKUU
YA UBATIZO WA BWANA
MWANZO:
Mat.
3:16-17
Bwana
alipokwisha kubatizwa, mbingu zikamfunukia, Roho akashuka kwa mfano wa hua, na
kukaa juu yake; na tazama, sauti ya Baba ikasema: Huyu ni Mwanangu, mpendwa
wangu, ninayependezwa naye.
SOMO
1
Isa.
42:1-4, 6-7
Bwana
asema: Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu
imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu.
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza
hukumu kwa kweli. Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu
duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. Mimi, Bwana, nimekuita katika haki,
nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya
mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale
walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
29:1-4, 9-10 (K) 11
(K)
Bwana atawabariki watu wake kwa amani.
Mpeni
Bwana, enyi wana wa Mungu,
Mpeni
Bwana utukufu na nguvu;
Mpeni
Bwana utukufu wa jina lake;
Mwabuduni
Bwana kwa uzuri wa utakatifu. (K)
Sauti
ya Bwana I juu maji
Bwana
yu juu ya maji mengi
Sauti
ya Bwana ina nguvu,
Sauti
ya Bwana ina adhama. (K)
Sauti
ya Bwana yawazalisha ayala,
Na
ndani ya hekalu lake wanasema wote, Utukufu.
Bwana
aliketi juu ya Gharika;
Naam,
Bwana ameketi hali ya mfalme milele. (K)
SOMO
2
Mdo.
10:34-38
Siku
ile: Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana
upendeleo, bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa nay
eye.
Neno
lile alilowapelekea wana wa Israeli, akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu
Kristo (ndiye Bwana wa wote), jambo lile ninyi mmelijua, lililoenea katika
Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliohubiri Yohane; habari za
Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu;
naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na
Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Mk.
9:7
Aleluya,
aleluya,
Mbingu
zilimfunguka na sauti ya Baba ikasikilika,
“Huyu
ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.”
Aleluya.
INJILI
Mk.
1:7-11
Siku
ile: Yohane alihubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi,
ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi
niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.
Ikawa
siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohane
katika Yordani. Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na
Roho, kama hua, akishuka juu yake; na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe
Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment