“MGEGU
ZA UZIMA”
Januari
10, 2021.
------------------------------------------------
JUMAPILI,
SHEREHE YA UBATIZO WA BWANA
Somo
la 1: Isa 42:1-4, 6-7 Nabii Isaya anatabiri juu ya unabii wa ujio wa mtumishi
wa Bwana ambaye Roho wa Bwana yuu ndani yake. Huyu ni Mteule wa Mungu na
anapendwa sana na Mungu. Kwa ujio wa Yesu maneno haya yalisikika Baba akiyasema
kuhusu Mwanae.
Wimbo
wa katikati: Zab. 29:1-4, 9-10 (K) 11, Mungu anahidi kuwabariki watu wake kwa
Amani. Kwa ujio wa Kristo Amani imeingia ulimwenguni.
Somo
la 2: Mdo. 10:34-38 Petro anashuhudia kwamba kwakweli Mungu hana upendeleo
wowote. Yesu amekuja ulimwenguni kwa ajili ya watu wote sio kwa ajili ya watu
wachache tu. Wale wote wanaokubali kuwa wake kwa ubatizo anawafanya wana wa
Mungu.
Injili:
Mk. 1:7-11 Tunasikia kuhusu hali ya Marko kuhusu ubatizo wa Yesu anaye batizwa
na Yohane Mbatizaji na kujidhihirisha kwa Utatu Mtakatifu.
UBATIZO
KAMA WA WATOTO WA MUNGU!
Sikukuu
ya leo, inamalizia kipindi cha Noeli na kuanza kipindi cha Mwaka wa Kanisa. Ni
sikukuu inayo onesha mpito wa Yesu kutoka katika utume wake uliofichika na
kuanza utume wa hadharani. Ubatizo wa Yesu una dhihirisha ‘Umungu wa Yesu kwa
wafuasi wote wa mwanzo na kwa wanafunzi wa yohane Mbatizaji.
Je,
ni kwanini Yesu aliruhusu Yeye mwenyewe kubatizwa? Hakuhitaji ubatizo, wala
kutubu kwani yeye hakuwa na dhambi. Siajabu Yohane Mbatizaji alishangazwa sana:
“Yohane anasema ninapaswa ni batizwe nawe, nawe umekuja kwangu mimi.” Yesu
alitaka kuonyesha umoja wake na wanadamu, kujihusisha mwenyewe moja kwa moja na
wanadamu wadhambi ili awaokoe kutoka dhambini. Kilikuwa ni kitendo chake
mwenyewe. Ubatizo wa Yesu unatabiri kifo chake mwenyewe, ufufuko na Ujio wa
Roho Mtakatifu kama Yohane alivyoweka: “Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na
moto.”
Ubatizo
wa Yesu ulikuwa ni wa lazima kwasababu kwake yeye ulikuwa ni muda wa maamuzi.
Ulitoa ishara kwa Yesu kuanza utume wake. Yesu anachukua changamoto
ya
Mungu kwa kufanya uamuzi wa kuanza utume wake ulimwenguni. Ubatizo wa Yesu
kwake Yeye ulikuwa ni wakati wa utambulisho. Ulikuwa ni muda kwake yeye
kujitambulisha mwenyewe pamoja na Mungu. Na Yesu anajua anafanya haya kwa ajili
yetu sisi. Ubatizo wa Yesu ulikuwa ni wakati wa kuthibitishwa kwake. Yesu
alikuwa tayari kuchukua utume wake na alipokea wakati huu wa thibitisho la
Mungu: “Huyu ni mwanangu mpendwa.” Ubatizo wa Yesu kwake yeye ulikuwa ni wakati
wa pekee. Mungu anatutaka sisi tumsikilize Mwanae. Sisi tujifunze kumsikiliza
Yesu katika maandiko Matakatifu, licha ya sauti mbali mbali zilizopo
Ulimwenguni, tujifunze kumsikiliza Yesu na kumchagua yeye pekee. Ujumbee
anaotangaza nabii Isaya katika somo la kwanza kuhusu mtumishi wa Mungu,
unatimilika ndani ya Kristo katika ukamilifu wote kama Injili inavyo
mdhihirisha. Ndivyo anavyo lidhihirisha hilo mtume Petro katika somo la pili,
kwamba Yesu ni mteule wa Mungu. Yeye anaponya madhaifu yote na kutufanya tuwe
kuru kwa kututoa gizani na kutufanya watoto wa Mungu.
Yesu
aliileta Habari Njema, ujumbe wa amani tofauti na ujumbe wa Yohane, Yesu yupo
tayari sasa kuushinda ulimwengu kwa upendo."Ubatizo Mtakatifu ni msingi wa
maisha yote ya Kikristo, mlango wa kuingilia uzima katika Roho, na mlango
unaowezesha kuzipata sakramenti nyingine." (Katekisimu ya Kanisa Katoliki
- 1213). Katika ubatizo wetu Mungu “anafungua mbingu” na anatutumia Roho wake
Mtakatifu; mbingu iliyofungwa kwa dhambi ya Adamu na Eva sasa imefunguliwa.
Katika ubatizo Roho Mtakatifu anachukua nafsi zetu, anazitakasa, na anazifanya
kuwa makao yake yanayofaa.
Kwetu
pia anasema katika ubatizo: “Huyu ni mwanangu mpendwa.” Ubatizo unatufanya sisi
kuwa watoto wakweli wa Mungu. Kama Yesu sisi pia tunapaswa kuongozwa na Roho na
kuwa tayari kutekeleza utume uliokabidhiwa kwetu. Maisha yetu yote yanapaswa
yawe “Habari Njema” kwa wengine, kwa kuwasaidia na kutenda mema, hususani kwa
wahitaji.
Sala:
Bwana, Nisaidie kutambua kuwa Mimi ni mwanao. Yesu nakuamini wewe. Amina.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment