MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 1, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 4 LA MWAKA
SOMO
13
Ebr.
11:32 – 40
Ndugu
zangu niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na
Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa Imani
walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa
vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa
nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya
wageni. Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa
vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; wengine
walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;
walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga;
walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa
wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa
nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango
na katika mashimo ya nchi. Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya Imani
yao, hawakuipokea ahadi; kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu
kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
31:19 – 23 (K) 24
(K)
Iweni hodari, mpige moyo konde, nyinyi nyote mnamngojea Bwana.
Jinsi
zilivyo nyingi fadhili zako
Ulizowawekea
wakuchao;
Ulizowatendea
wakukimbiliao
Mbele
ya wanadamu. (K)
Utawasitiri
na fitina za watu
Katika
sitara ya kuwapo kwako;
Utawaficha
katika hema
Na
mashindano ya ndimi. (K)
Bwana
ahimidiwe;
Kwa
maana amenitendea fadhili za ajabu
Katika
mji wenye boma. (K)
Nami
nalisema kwa haraka yangu,
Nimekatiliwa
mbali na macho yako;
Lakini
ulisikia sauti ya dua yangu wakti nilipokulilia. (K)
Mpendeni
Bwana, ninyi nyote mlio watauwa wake.
Bwana
huwahifadhi waaminifu,
Humlipa
atendaye kiburi malipo tele. (K)
SHANGILIO
Yn.
15:15
Aleluya,
aleluya,
Bwana
anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote
niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
INJILI
Mk.
5:1 – 20
Yesu
na wanafunzi wake walifika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. Na
alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini,
mwenye pepo mchafu; makao yake yalikuwa pale makaburini; wal ahakuna mtu yeyote
aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara
nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile
pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na
mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakatia kwa
mawe.
Na
laipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti
kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa
Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu.
Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.
Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. Na hapo milimani palikuwa na kundi
kubwa la nguruwe, wakilisha. Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika
nguruwe, tupate kuwaingia wao. Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka,
wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni,
wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.
Wachungaji
wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashamba. Watu wakatoka walione
lililotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa
nguo, ana akili zake, ndiye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye
ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza
ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. Wakaanza
kumsihi aondoke mipakani mwao.
Naye
alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja
naye; lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu
wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi
alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani
makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment