“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Februari 1, 2021
Juma
la 4 la Mwaka wa Kanisa
Ebr
11: 32-40;
Zab
31: 20-24;
Mk
5: 1-20.
KUBADILISHWA
NA YESU!
Ndugu
zangu karibu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Tuanze tafakari
yetu kwa kuangalia zaburi ya wimbo wa katikati inayotualika tuwe hodari na
kupiga moyo konde hasa sisi ambao tunamngoja Bwana. Zaburi hii inatuasa kwamba
ulimwenguni kuna changamoto nyingi na wakati mwingine maisha yanatawaliwa na
hali ya kukata tamaa. Hivyo tunaambiwa tuwe hodari, tusiwe legelege tunapaswa
tuwe na imani.
Imani
imewasaidia wengi kupigana hata na mambo yasiyowezekana, somo la kwanza
linataja watu mbalimbali ambao maisha yao yalijaa imani wakafanikiwa kwa kila
jambo. Walipata maadui wengi, walikutana hata na simba lakini kwasababu ya
imani yao kwa Mungu walishinda.
Sisi
nasi ndugu zangu tunateseka sana na kuyumbishwa na kila upepo wa ulimwengu
kwasababu hatuna imani. Imani yetu imekuwa haba, tunatishiwa na vitu vidogo
tunaogopa hata kumwacha Mungu. Tukiumwa kidogo tunazunguka kwa waganga mbali
mbali, tunalishwa kila aina ya uchafu na masharti makali. Tujue wakutegemea ni
Mungu, imani yetu ni muhimu sana, tuwe hodari.
Katika
somo la Injili Yesu anamtoa pepo mchafu ambaye alikuwa akimtesa mtu kwa muda
mrefu. Wengi walihangaika naye hata kumfunga lakini hawakuweza. Hili ni
fundisho kwamba tunaweza pia kuhangaika na baadhi ya mambo au changamoto
kwakutegemea watu lakini hatuwezi kufanikiwa kama Yesu hana nafasi.
Tumkaribishe
Yesu, tuna matatizo mengi ambayo twaweza kuyafananisha na lile kundi la Pepo
mchafu, ambayo yanatufunga na kututesa, tunahangika mnoo, na tumesahau kwamba
Yesu ndiye msaada wetu. Twende kwake, tuwe hodari katika imani, sisi anatupenda
kuliko viumbe vingine vyote, sisi ni wana wa Mungu ndio maana nguruwe wale
hawakuwa muhimu kuliko mwanadamu. Yesu anatupenda sana tuwe na imani.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment