ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 12, 2020.
------------------------------------------------
JUMAMOSI, JUMA LA 2 LA
MAJILIO
Somo la 1: Ybs 48: 1-4,
9-11 maisha ya Elia yanasifiwa na mwandishi wa Kitabu cha Yoshua Bin Sira.
Alihubiri toba, alichukuliwa mbinguni na alikuwa mpatanishi
Wimbo wa katikati: Zab
79: 2-3, 15-16, 18-19; Bwana tunakuomba uso wako utuangaze nasi tutakuwa
salama. Tunakuomba utupe uzima nasi tutaliita jina lako.
Injili: Mt 17: 10-13
Yesu, akiongelea kuhusu mapokeo kwamba Elia atakuja tena, Yesu anasema kwamba
tayari ameshakuja katika ujio wa Yohane Mbatizaji lakini alikataliwa.
------------------------------------------------
YAHWEH NI MUNGU WETU
Elia alikuwa akitazamiwa
kurudi ulimwenguni kabla ya mwisho wa nyakati na kabla ya kuja kwa Masiha. Watu
hawakuwa na uhakika. Kama Yohane Mbatizaji alikuwa ndiye Elia ajae ulimwenguni,
basi Yesu ni Masiha, anayekuja kipindi cha mwisho cha ulimwengu. Yesu anajibu
swali la wafuasi kwamba Yohane Mbatizaji kweli yeye ndiye Elia aliyerudi ulimwenguni.
Kazi ya Yohane Mbatizaji
kama Elisha aliyekuja Waandishi walishindwa kuiona. Walishindwa kumuona yeye
akitimiza kazi ya Elisha ya kuandaa njia kwa ajili ya Bwana. Kama Yohane
alivyokuwa na kazi ya pekee ya kumtambulisha na kuandaa njia kwa ajili ya ujio
wa Kristo, sisi pia tuna kazi ya kumkaribisha Yesu daima. Yesu alikuja miaka
mingi iliopita, lakini daima anatamani kuja daima katika maisha yetu. Na
anaweza kuja tu kama tumejiandaa vizuri.
Ujumbe mkuu wa Yohane ni
kutubu dhambi zetu. Ingawaje sisi wote tunakazana kujikinga na dhambi,
kwasababu ya matokeo ya kuanguka kwa Mwanadamu, hatupaswi kusahau kwamba wito
wetu ni kuwa wakamilifu, kuwa wakamilifu kama Baba yetu wa Mbinguni alivyo
mkamilifu. Tunaitwa kutambua dhambi zetu, kuziungama, na kujitahidi kujinasua
kutoka kwenye dhambi hizo.
Kipindi cha majilio ni
kipindi muhimu cha kufanya hivyo daima, na ni muhimu kutafuta neema
zinazopatikana kwa neema ya Sakramenti ya kitubio katika kipindi hiki
kitakatifu. Tujitazame wenyewe katika mioyo yetu ni kwa jinsi ghani tulivyo
tayari kuihubiria mioyo yetu kuhusu kutubu na kuacha dhambi. Kukubali toba
kutubu kipindi hiki ni kitu chema kabisa ambacho twaweza kufanya ili kuandaa
kuja kwa Kristo daima katika maisha yetu.
Sala: Bwana, nisaidie niweze
kuziona dhambi zangu kadiri tunavyozama katika kipindi hichi cha majilio.
Nisaidie niweze kutambua yale yote yanayonifanya niwe mbali nawe na kuyaacha
kwa moyo wote. Yesu nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment