“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne,
Desemba 22, 2020,
Juma
la 4 la Majilio
1
Sam 1: 24-28;
1
Sam 2: 1, 4-8;
Lk
1: 46-56
MSIFU
MUNGU KILA WAKATI!
Ndugu zangu karibuni katika adihimisho la
Misa Takatifu asubuhi ya leo. Katika tafakari ya masomo yetu ya leo, tunakutana
na kina Mama wawili waliojaa furaha na shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo
makuu aliyowatendea.
Somo la kwanza lamhusu mama yake Samweli.
Yeye alionja ugumu na uchungu wa kukaa bila mtoto, huku akisengenywa na
kudharauliwa na wanawake wenzake. Bwana alimtendea makuu na leo amekuja
kushukuru wema wa Bwana aliomtendea.
Mama Maria na yeye amejaa shukrani kwa
Mungu kwa makuu aliyomtendea ya kuwa Mama wa Masiha. Hii ni nafasi
iliyotamaniwa na kila mwanamama ndani ya taifa la Israeli. Sasa kiajabu
inamuangukia Maria na yeye hana cha kufanya bali ni kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Moyo wa shukrani unapingana na uchoyo.
Ukiwa mchoyo kwa Mungu, tusipotoa shukrani kwake ndio sababu zetu sisi kuanguka
ndugu zangu na kushindwa kulinda kile kidogo tulichokipata. Ukweli ni kwamba
Mama yake Samweli aliongezewa zaidi watoto wengine kwa kitendo chake cha yeye
kuja na kumtolea Mungu shukrani. Mungu alimfungulia milango ya fanaka tele. Na
Mama Maria alifunguliwa milango ya fanaka tele kwa kitendo chake cha kutoa sala
hii ya shukrani.
Sisi tuyalinde mafanikio yetu kwa moyo wa
shukrani zaidi. Mafanikio yasituletee kujivuna au kumkana Mungu au kuacha
kutambua nafasi yake kwetu. Mafanikio yanalindwa kwa njia ya sala. Kuacha
kusali kwa sababu ya kiwewe kiletwacho na mafanikio imetunyima mengi.
Leo ni siku ya kuchunguza yote niliyoacha
kumrudishia Mungu kama shukrani na kumpatia nafasi yake. Nitambue kwamba hali
yangu imezidi kuwa mbaya kutokana na kutojitambua kwamba ninapaswa kumrudishia
Mwenyezi Mungu shukrani. Kumbuka ukipiga magoti na kuomba kitu, ukipata
usisahau kutoa shukrani kwa Mungu. Tumsifu Yesu Kristo.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment