“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Desemba 24, 2020,
Juma la 4 la Majilio
2 Sam 7: 1-5, 8-12, 14, 16;
Zab 88: 2-5, 27, 29;
Lk 1: 67-79
MATAMANIO YAKO YATAKATIFUZWE!
Jioni ya Kuzaliwa kwa Bwana Yesu,
liturujia inatukumbusha sisi kuwa hakika Mungu anasikiliza sala zetu na
anazitekeleza sala zote. Ndoto zetu zote na ndoto kubwa za kumuangalia muumbaji
pia zinakamilishwa na Mungu.
Katika somo la kwanza Mungu analikataa
wazo la Daudi la kulijenga Hekalu la Bwana na alizitoa sababu tatu. Kwanza,
hakukuwa na uhitaji kwani sanduku la agano lilihifadhiwa katika vibanda tokea
Kutoka. Pili, Mungu hakuwaamuru watu wake wamjengee Yeye hekalu la kudumu.
Tatu, Daudi alikuwa hastahili kulijenga hekalu kwasababu yeye alimwaga damu
nyingi. Mungu alikuwa hamuadabishi Daudi wala kumkataa yeye bali alikuwa tu
anaziongoza tena huduma zake. Alitakiwa awe kiongozi, sio mjenga hekalu.
Vile vile, daima Mungu haturuhusu sisi
kuyachukua matamanio yetu. Wakati mwingine Yeye anafanya kutowezekana kwasababu
anahitaji sisi tumtumikie Yeye katika njia nyingine. Utambuzi wa ukweli huu
utawasadia wakristo wengi kujua yasiyo ya kweli na ndoto zakuogopesha.
Sala: Bwana, niongoze mimi katika njia
Yako, maisha yangu kadiri ya mipango Yako. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment