MASOMO
YA MISA JANUARI 1, 2021
SHEREHE
YA MARIA MTAKATIFU MAMA WA MUNGU
SOMO
1
Hes.
6:22-27
Bwana
akanena na Musa, na kumwambia, Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo
mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia; Bwana akubarikie, na kukulinda;
Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na
kukupa Amani. Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami
nitawabarikia.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
67:1-2,4,6-7 (K) 1
(K)
Mungu na atufadhili na kutubariki.
Mungu
na atufadhili na kutubariki,
Na
kutuangazia uso wake.
Njia
yake ijulikane duniani,
Wokovu
wake katikati ya mataifa yote. (K)
Mataifa
na washangilie,
Naam,
waimbe kwa furaha,
Maana
kwa haki utawahukumu watu,
Na
kuwaongoza mataifa walioko duniani. (K)
Nchi
imetoa mazao yake;
Mungu,
Mungu wetu, ametubariki.
Mungu
atatubariki sisi;
Miisho
yote ya dunia itamcha Yeye. (K)
SOMO
2
Gal.
4:4-7
Ndugu
zangu: ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa
na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya
sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Na kwa kuwa ninyi mmekuwa
wana. Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana na kama u mwana, basi, u mrithi
kwa Mungu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
INJILI
Lk.
2:16-21
Siku
ile: Wachungaji wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto
mchanga amelala horini. Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo
mtoto. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji. Lakini
Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. Wale wachungaji
wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na
kuyaona, kama walivyoambiwa. Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa
jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment