“MBEGU
ZA UZIMA”
Ijumma
, Januari 1, 2021,
SHEREHE
YA MARIA, MAMA WA MUNGU
Hes
6:22-27;
Zab
67: 1-2, 4, 6-7;
Gal
4:4-7;
Lk
2:16-21
MAMA
MARIA, MLINZI NA KIONGOZI WETU!
Katika
somo la kwanza, baraka ya Mungu kwa watu wake imeainisha tumaini kwao.
Ilimaanisha ushujaa wa kuyashinda matatizo ya kila siku za maisha. Leo sisi pia
tunaobwa tutumaini katika Bwana na kuomba baraka zake mwanzo wa mwaka huu.
Katika somo la pili, Paulo anatupatia sisi sababu za kuwa na tumaini katika
mwanzo wa Mwaka Mpya: Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, ambaye amekuwa mmoja
pamoja nasi; alikuwa kaka yetu, katika kila kitu kama sisi isipokuwa katika
dhambi. Mungu ametukubali sisi kama watoto Wake. Sisi Wakristo tunapaswa
kushuhudia upendo wa Mungu ukidhihirishwa kwa Yesu Kristo. Pia leo, Kanisa
linasherehekea sikukuu ya Maria, Mama wa Mungu. Mama Kanisa anajali sana kiasi
cha kuwa na mfano ulio bora wa kuigwa kwa mwaka mzima na hivyo anatupa sisi
Mariamu, Mama wa Yesu katika siku ya kwanza ya mwaka. Kadiri siku inavyoanza na
Mwaka Mpya unaanza, sisi hatupo pekeyetu; tunaye Mama Mkombozi ili atulinde na
atuongoze sisi kwa mwaka wote.
Ndani
ya Yesu kuna asili mbili – ya kibinadamu na ya kimungu, lakini yeye ni mtu
mmoja. Mariamu ambaye pia ni Mama wa Mungu. Alikuwa na nafasi ya pekee sana ya
kuutoa mwili na damu yake kwa Yesu. Mariamu anachukua nafasi katika kazi ya
ukombozi kazi ya Kristo pamoja na upendeleo wa pekee kiasi cha kuwa hata
malaika wa mbinguni wangekuwa na wivu. Kati ya viumbe vyote vya Mungu ulimwenguni
na mbinguni, hakuna hata mmoja aliye mtakatifu sana na aliye karibu sana na
Yesu zaidi ya Mariamu, Mama Yake. Mama Maria ni Eva Mpya. Eva, mama wa wanadamu
alileta kifo kutokana na kutokutii kwake, kwake yeye mwenyewe na kwa wanadamu
wote, lakini Mariamu Eva Mpya, alileta uhai kutokana na kutii kwake. Mt.
Ireniusi alimuita Mariamu kuwa ndiye chanzo cha Ukombozi wetu. Kadinali Newman aliyetoa tofauti kati ya
Mariamu na Eva alisema, “Kama eva alivyoipoteza nafasi ya upendeleo kutokana na
Dhambi, hivyo Mariamu aliipata nafasi ya upendeleo kutokana na matunda ya
neema; Kama Eva alivyokosa kutii na asiyeamini, hivyo Mariamu alikuwa mtii na
aaminiye; kama Eva alivyokuwa ni chanzo cha kuanguka kwa wote, Mariamu alikuwa
ni chanzo cha ukombozi kwa wote; kwamba Eva aliandaa mazingira ya kuanguka kwa
Adamu, hivyo Mariamu aliandaa mazingira ya kuweka hali sawa kwa Bwana; hivyo,
ambapo zawadi ya bure haikuwa ni dhambi bali ni bora zaidi, inafuata kuwa, kama
Eva alisaidia katika kutekeleza dhambi kubwa, Mariamu alisaidia katika
kutekeleza kile kilicho bora zaidi. Mariamu ni zawadi kubwa sana kutoka kwa
Yesu kwetu sisi. Yesu alifahamu kuwa Mama Yake alikuwa mkuu na kama ni zawadi
ya mwisho, alimtoa Mariamu kwetu sisi kama mama yetu.
Sala:
Mariamu, nifundishe mimi kusema Ndiyo kwa Bwana. Amina
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment