MASOMO
YA MISA DESEMBA 9, 2020
JUMATANO,
JUMA LA 2 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
40:25-31
Mtanifananisha
na nani, nipate kuwa sasa naye? Asema yeye aliye Mtakatifu. Inueni macho yenu
juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita
zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu
zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.
Mbona
unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana
asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? Je! Wewe hukujua?
Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala
hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu
yeye asiyekuwa na uwezo. Haya vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana
wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa
mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala
hawatazimia.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
103:1-4,8,10 (K) 1
(K)
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Ee
nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Naam,
vyote vilivyo ndani yangu,
Vilihimidi
jina lake takatifu.
Ee
nafsi yangu umhimidi Bwana,
Wala
usizisahau fadhili zake zote. (K)
Akusamehe
maovu yako yote,
Akuponya
magonjwa yako yote,
Aukomboa
uhai wako na kaburi,
Akutia
taji ya fadhili na rehema. (K)
Bwana
amejaa huruma na neema,
Haoni
hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Hakututenda
sawasawa na hatia zetu.
Wala
hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Tazama
Bwana atakuja kuwaokoa watu wake, Heri walio tayari kumlaki.
Aleluya.
INJILI
Mt.
11:28-30
Siku
ile, Yesu alijibu akasema: Njoni kwangu nyote msumbukao na wenye kulemewa na
mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi
ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana
nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment