MASOMO
YA MISA DESEMBA 30, 2020
SIKU
YA SITA YA OCTAVA YA KUZALIWA BWANA
SOMO
1
1Yoh.
2:12-17
Nawaandikia
ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina
lake. Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu
mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu.
Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba. Nimewaandikia ninyi,
akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi,
vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi
mmeshinda yule mwovu.
Msiipende
dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba
hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na
tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na
dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya
Mungu adumu hata milele.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
96:7-10 (K) 11a
(K)
Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie
Mpeni
Bwana, enyi jamaa za watu,
Mpeni
Bwana utukufu na nguvu,
Mpeni
Bwana utukufu wa jina lake. (K)
Leteni
sadaka mkaziingie nyua zake,
Mwabuduni
Bwana kwa uzuri wa utakatifu,
Tetemekeni
mbele zake, nchi yote. (K)
Semeni
katika mataifa, Bwana ametamalaki;
Naam,
ulimwengu umethibitika usitikisike,
Atawahukumu
watu kwa adili. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya
Siku
takatifu imetung’aria: Enyi mataifa njoni mkamwabudu Bwana: Kwa sababu mwanga
mkubwa umeshuka duniani.
Aleluya.
INJILI
Lk.
2:36-40
Siku
ile palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri,
na umri wake ulikuwa miaka mingi alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya
uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika
hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu alitokea saa
ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika
Yerusalemu akawatolea habari zake.
Basi,
walipokwisha kuyatimiza yote kama yaliyoagizwa katika sheria ya Bwana,
walirejea Galilaya, mpaka mjini kwao, Nazareti. Yule mtoto akakua, akaongezeka
nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment