“ASALI
ITOKAYO MWABANI”
Desemba
30, 2020.
------------------------------------------------
JUMATANO,
OKTAVA YA NOELI
Somo
la 1: 1 Yn 2:12-17 Yohane anaendelea kutuhubiria sisi tena na kutukumbusha juu
ya jukumu letu kama Wakristo, na hasa juu ya sisi kuwa macho kwasababu ya
malimwengu.
Wimbo
wa Katikati Zab: Ps 95: 7-10 Mbingu na zifurahi nchi na ishangilie. Mwabuduni
Bwana hekaluni mwake. Ee Dunia tetemeka mbele za Bwana.
Injili:
Lk 2: 36-40 Anna, nabii mwanamke, anasali kwa ujasiri kama Simeoni kwa ajili ya
Mkombozi. Wakati alipo muona, na kumpa Mungu shukrani na anaondoka na kwenda
kumwambia kila mmoja kuhusu hili.
------------------------------------------------
JIBU
LA KUKUMBANA NA KIPINDI CHETU CHA NOELI
Leo
katika siku ya sita ya oktava ya Noeli, tunamheshimu nabii Anna. Jana Semoni
aliye oneshwa kama “mtu wa hekima na busara” ambaye alisubiria mpaka siku ya
mwisho na kumuona Masiha. Leo pia tuna jambo kama hilo, Anna anasifika kwa
ujasiri wake, na huduma yake katika hekalu, akisali na kufunga. Alikuwa ni
mjane na ilikuwa ni miaka saba tu baada ya kuolewa, na alikuwa akitumikia
katika hekalu karibia nusu ya karne moja. Ingawaje angeweza hata kuomba udhuru
kwasababu ya umri wake, Anna alijitoa mwenyewe daima katika sala na kufunga.
Hakuna sehemu yoyote katika Agano jipya tunasoma kuhusu “nabii Mwanamke”
msemaji wa Mungu, ni Anna pekee.
Aliweza
kutambua ujio wa Bwana kwasababu ya kujaliwa neema na Mungu, alitambua ujio
wake baada ya kupelekwa hekaluni na Maria na Yosefu. Tunaona uzuri uliopo katika
jibu la Anna. “Anaongea kuhusu Mtoto kwa wale wote waliokuwa wakimsubiri mtoto
na mkombozi wa Yerusalemu”. Anna anawakilisha waumini wa kweli kwa njia ya
sala. Huduma yake kwa hekalu na kutangaza kwake habari njema kuhusu Yesu.
Tunapata
somo kubwa sana kwetu kuhusu kukutana kwake na Yesu. Tunapokutana na Yesu
katika maisha yetu ya Imani na sala, je tunapata furaha ya kushirikisha kwa
wengine? Pengine kwa njia ya maneno yetu lakini zaidi mara nyingi kwa kuwa
mashahidi wake. Ukweli ni kwamba maana halisi ya Noeli inapaswa kushirikishwa
kwa wengine. Inapaswa kushirikishwa katika ulimwengu mzima na kutambua ujio wa
Masiha ulimwenguni.
Tafakari,
juu ya nabii Anna. Jaribu kufikiria juu ya furaha yake alivyokuwa akimuona huyu
Mfalme aliyezaliwa. Sali ili hali kama yake ikupate uweze kumtangaza Kristo kwa
maisha yako na kumfanya Mungu awe njia katika njia yako.
Sala:
Bwana, ninakuomba niweze kufahamu maana halisi ya Noeli. Ninakuomba niweze
kuhifadhi furaha hii ya kuzaliwa kwako katika moyo wangu. Ninakuomba niweze
kuishi zaidi kwa makini na katika Imani ninaposhiriki katika mafumbo haya ya
Noeli. Yesu nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment