MASOMO YA MISA DESEMBA 25, 2020
SHEREHE YA KUZALIWA BWANA
SOMO 1
Isa. 52:7-10
Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima, miguu
yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye Amani, aletaye habari njema ya
mambo mema, yeye atangazaye wokovu, auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!
Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja; maana wataona jicho
kwa jicho, Jinsi Bwan arejeavyo Sayuni. Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja,
enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa Bwan amewafariji watu
wake, Ameukomboa Yerusalemu. Bwana ameweka wazi mkono wake mtakatifu machoni pa
mataifa yote; Na ncha zote za dunia zitauona wokovu wa Mungu wetu.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 98:1-6 (K) 3
(K) Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa
Mungu wetu.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
(K)
Bwana ameufunua wokovu wake,
Machoni pa mataifa amedhihirisha haki
yake,
Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.
(K)
Miisho yote ya dunia imeuona,
Wokovu wa Mungu wetu,
Mshangilieni Bwana nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni
zaburi. (K)
Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi,
Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
Kwa panda na sauti ya baragumu,
Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana. (K)
SOMO 2
Ebr. 1:1 – 6
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu
katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi
amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye
aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi
yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa
dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; amefanyika bora kupita
malaika, kwa kadiri ya jina alilorithi lilivyo tukufu kuliko lao.
Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati
wowote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, mimi nitakuwa kwake baba,
Na yeye atakuwa kwangu mwana? Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza
ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Aleluya, aleluya!
Siku takatifu imetung’aria: enyi mataifa
njoni mkamwabudu Bwana, kwa sababu leo mwanga mkubwa umeshuka duniani.
Aleluluya.
INJILI
Yn. 1:1-18
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno
alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.
Ndani yake ndimo ulikuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru
yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu,
jina lake Yohane. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate
kuamini kwa yeye. Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.
Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila
mtu, akija katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu
ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala wali wake
hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu,
ndio wale walioaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi
ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili,
akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye
kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Yohani alimshuhudia, akapaza sauti yake
akasema. Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa
mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi
sote tulipokea, na neema juu ya neema. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa
Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona
Mungu wakati wao wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu
ndiye aliyemfunua.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment