“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 25, 2020,
SHEREHE YA KUZALIWA BWANA
Isa 52: 7-10;
Zab 98: 1-6;
Ebr 1:1-6;
Yn 1: 1-18
HURUMA IMEPATA KUWA HAI!
Huruma imepata kuwa hai na yenye kuonekana
katika Yesu Mnazareti, na hata ikafikia kilele chake katika Yeye. Baba “aliye
mwingi wa rehema” (Efe 2:4), baada ya kumfunulia Musa jina lake kuwa ni “Mungu
mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli”
(Kut 34:6), hakuwahi kuacha hata mara moja kuonyesha hali yake ya kimungu
katika nafasi zote za historia. “Ulipowadia utimilifu wa wakati” (Gal 4:4),
kila kitu kilipokuwa kimepangwa kadiri ya utaratibu wake wa ukombozi, alimtuma
duniani Mwanae pekee ili kutufunulia upendo wake katika ukamilifu wake.
Huruma ni chemchemi ya furaha, ya utulivu
na ya amani. Ni sharti la wokovu wetu. Huruma ni tendo la juu na kuu kabisa
ambalo kwa njia yake Mungu anatujia sisi. Huruma ni njia inayowaunganisha Mungu
na binadamu, na kuufungulia moyo mlango wa matumaini ya kupendwa daima, licha
ya hali yetu ya dhambi. (Rej. BULA YA KUZINDUA JUBILEI YA PEKEE YA HURUMA 1,2)
Leo Kanisa pamoja na viumbe vyote vyajawa
na furaha kwani vimefanywa upya na kuwa kiumbe kipya kwa njia ya kuzaliwa kwa
Bwana wetu Yesu Kristo. “Neno” basi na uwe mwanga (Mwa. 1:3), lililoleta
uumbaji sasa limeongelewa tena, kupitia kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mkombozi
wetu. Mwanga (Yn. 1:8), sasa anang’ara katika giza. Mwanga, atoaye mwanga kwa
kila mtu amekuja ulimwenguni. Mungu asiyefahamika, sasa amefanywa afahamike,
Baba sasa anajidhihirisha mwenyewe, kupitia mwanae wa kiume, Yesu. Neno
alifanyika mwili na akakaa kwetu.
Umwilisho au Noeli ni sherehekeo la furaha
hii – Mungu wetu anakuwa mwili na anakuja kukaa ndani yetu wanadamu. Tukio hili
liliufanya ulimwengu ufurahi , malaika walifurahi kwa Utukufu kwa Mungu,
waliomba kwaajili ya amani duniani kwa watu. Ingawa ukaribisho wa Bwana Yesu
haukuwa wa furaha sana ulimwenguni. Mkombozi hakuwa na nafasi ya kuzaliwa, bali
katika uhakika, katika moja ya vijiji vidogo Bethlehemu. Hakuwa na tafrija ya
ukaribisho, isipokuwa tu kwa baadhi ya wanyama katika hali ya ukimya na baadae
wachungaji wachache waliomuabudu Yeye. Mfalme Herode alimchukulia mtoto kuwa kama
ni tishio, alitaka mtoto Yesu auwawe. Katika miaka ya mbeleni, mkombozi wetu
alikanwa, alivamiwa na kusulubiwa. Na kwa hayo yote aliyoyapokea, mkombozi
pekee alirudisha huruma, huruma na upendo. Leo, Yesu amezaliwa kati yetu tena,
katika hali yetu ya kumkana na hali ya dhambi; Yeye amezaliwa Bethlehemu ya
hali ya ubinafsi, umimi, mateso, vita, unyonyaji, nakadhalika. Je, sisi tupo
kama wachungaji, waliokwenda kwa Yesu na kuzitoa heshima zao au tupo kama
Herode, aliyemchukua Yesu kuwa kama ni tishio la uhuru wetu, katika hangaiko la
kutafuta starehe? Je, tunakwenda
kufurahi pamoja na wachungaji au kupanga mabaya kama Herode?
Katika milongo miwili iliyopita, dunia
yetu imekuwa nzuri sana kwa wanadamu pamoja na uwepo wa kimungu wa Mungu
mwenyewe. Ndani yake pia, wengi wametamani kuwa katika giza. Kwa namna ya
pekee, Yesu anahitaji azaliwe ndani yetu, awe Neno liletalo, mwanga unaoondoa
giza lote, huruma inayo futa dhambi zetu. Je, tupo tayari kujitoa wenyewe kwake
Yeye? Je, tupo tayari kuufahamu mwanga huo? Je, tupo tayari kupokea huruma
yake?
Sala: Bwana Yesu, nakuhitaji Wewe uzaliwe
ndani yangu leo, Nahitaji huruma yako inifanye chombo kikamilifu kwako.
Ninahitaji kunena juu yako katika maneno na maisha yangu. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment