MASOMO YA MISA DESEMBA 10,
2020
ALHAMISI, JUMA LA 2 LA
MAJILIO
KUMBUKUMBU YA MT. YOHANE
WA MSALABA,
PADRE NA MWALIMU WA
KANISA
SOMO 1
Isa. 41:13-20
Kwa maana mimi, Bwana,
Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi
nitakusaidia. Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi
nitakusaidia, asema Bwana, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli. Tazama,
nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha
milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi. Utawapepeta, na
upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia Bwana,
utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli.
Maskini na wahitaji
wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, Bwana,
nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.
Nitafunua vijito vya maji
juu ya vilima, na chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza jangwa kuwa ziwa la
maji, na mahali pakavu kuwa vijito vya maji.
Nitapanda katika jangwa
mwerezi, mshita, mhadasi, na mbono; nitatia katika nyika mberoshi, mtidhari, na
mteashuri pamoja; ili waone, na kujua wakafikiri, na kufahamu pamoja, ya kuwa
mkono wa Bwana ndio uliofanya jambo hilo. Mtakatifu wa Israeli ndiye
aliyeliumba.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 145:1,9-13 (K) 8
(K) Bwana ana fadhili, ni
mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.
Ee Mungu wangu, Mfalme
nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako
milele na milele.
Bwana ni mwema kwa watu
wote,
Na rehema zake zi juu ya
kazi zake zote. (K)
Ee Bwana, kazi zako zote
zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako
watakuhimidi,
Wataunena utukufu wa
ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza
wako. (K)
Ili kuwajulisha watu
matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya
ufalme wake.
Ufalme wako ni ufalme wa
zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya
vizazi vyote. (K)
SHANGILIO
Isa. 45:8
Aleluya, aleluya,
Dondokeni, enyi mbingu
toka juu, Mawingu yamwage haki; nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu.
Aleluya.
INJILI
Mt. 11:11-15
Siku ile, Yesu aliwaambia
makutano: Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazo wa wanawake aliye mkuu
kuliko Yohane Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu
kuliko yeye. Tangu siku za Yohane Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni
hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati
walitabiri mpaka wakti wa Yohane. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya
atakayekuja.
Mwenye masikio, na
asikie.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment