“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 10, 2020.
ALHAMISI, JUMA LA 2 LA
MAJILIO
Kumbukumbu ya Mt. Yahane
wa Msalaba, Padre na Mwalimu wa Kanisa,
Somo la 1: Isa 41:13-20
Mungu anajiita mwenyewe kwamba “Ni Mtakatifu pekee wa Israeli na kuwahakikishia
watu wakiwa katika mateso, anawaahidi upendo wake na kuwajalia na kutangaza
utukufu wake na wao kuufurahia.
Wimbo wa Katikati: Zab
144:1, 9-13 Mungu ni mkarimu na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni
mwingi wa mapendo. Yeye ni ufalme wa milele na utawala wake utatawala milele,
kutoka karne hata karne.
Injili: Mt 11: 11-15 Yesu
anamtambulisha Yohane Mbatizaji, anamuita mkuu kati ya wazawa wa wanawake, Elia
ambaye alikuwa aje.
------------------------------------------------
JE, UNAHITAJI MSAADA WA
MUNGU?
Kipindi cha majilio ni
kipindi cha kutazamia na kutamani ujio wa Bwana, ni kipindi cha kutamani ujio
wa Mungu hata Mungu mwenyewe anatamani sisi tuwe nae zaidi. Katika somo la
Kwanza katika kitabu cha nabii Isaya, Mungu anahitaji kutambuliwa kwa yote
ambayo amewatendea watu wake. Mungu anahimiza juu ya uhusiano: “mimi ni Bwana,
Bwana Mungu wako, ambaye ninatambua mkono wako wa kuume ”. Mungu anatuita sisi
kwa ujasiri wetu vilevile. Mara 11, Mungu ameonesha hilo “nitakusaidia”, nitakufanya
kuwa mkuu…”nitakujibu..”nitajifunua….” “kwa Ukarimu,” “Mimi”, Mungu anaonesha
kutaka kusaidia. “Ninataka kufanya mengi kwa ajili yako”.
Injili ya leo Yesu
anaongelea kuhusu Yohane mbatizaji. Yohane alifungwa kwasababu ya kumkemea
Herode, na hivyo akafungwa gerezani. Yesu anashuhudia utume wa Yohane na
kumuongelea kama mtu mkuu. Lakini Yesu anadhihirisha kwa kusema kwamba walio
wadogo katika ufalme wake ni mkuu zaidi kuliko Yohane. Aliye mdogo katika
kumfuata Yesu na mwenye neema ya Yesu ni mkuu kuliko Yohane Mbatizaji, katika
mambo ya kiroho na kushiriki kwake katika ufunuo wa yale yaliofunuliwa kwa
mafumbo ya Ufalme wa Baba. Hili halina maana kwamba sisi ni watakatifu kuliko
Yohane, au kwamba tunampendeza Mungu zaidi, au kwamba sisi ni muhimu zaidi
katika historia au katika kanisa kuliko huyu Mtangulizi wa Kristo. Yesu
alimaanisha kwamba sisi tunaufahamu mkubwa kuhusu ukombozi na kwamba tuna
nafasi ya kushiriki kwa undani ndani ya Bwana kwani tumepokea ukamilifu wa
Habari njema.
Je tunafanyaje hili? Je
tunahitaji msaada wa Mungu, ukombozi wake tunauhitaji? Mungu anahitaji kufanya
makuu kwa ajili yako. Kwa Yesu, Masiha, alikuja kutukomboa sisi. Je,
tunapokeaje utajiri wake?
Sala: Bwana, upo karibu.
Wewe ni mkarimu na mwenye huruma, hukasiriki haraka mwingi wa huruma.
Ninakuomba nifahamu unavyotamani mimi niwe nawe, ninakuomba niweze kuwa na
shauku hiyo hiyo ya kutimiza mapenzi yako. Yesu nakuamini wewe. Amina.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment