“MBEGU ZA UZIMA”
Desemba 27, 2020.
------------------------------------------------
JUMAPILI, OKTAVA YA NOELI
SIKUKUU YA FAMILIA TAKTIFU
Somo la 1: YbS 3:3-7, 14-17 Yoshua Bin
Sira anaweka mfano wa familia kutoka katika Agano la kale, mfano ambao
unasisitiza kuhusu majukumu ya kawaida na thawabu iliyowekwa kwa wale ambao
watatimiza jukumu hilo. Ni mkazo kuhusu jukumu la mmoja kuwaheshimu Baba na
Mama. Hili halina maana ya kuwaheshimu tu wakati tukiwa wadogo bali kuwatunza
pia wakati wakiwa wazee.
Wimbo wa Katikati: Zab 127: 1-5
Wamebarikiwa wale wenye hofu ya Bwana, wao na familia zao watabarikiwa na
watafanikiwa.
Somo la 2: Kol 3:12-21 Mfano mzuri wa
familia kadiri ya Paulo umejikita katika upendo na kuheshimiana kati ya kila
mmoja katika familia. Anasisitiza kwamba hali ya upendo inapaswa kuvuma katika
familia ya Kikristo, kwa msisitizo juu ya msamaha wa kila siku.
Injili: Lk 2: 22-40 inahusisha tukio la
kutolewa Bwana hekaluni, na linatueleza kidogo juu ya maisha yake huko
Nazareti.
*(Tunatumia masomo kutoka katika shajara
kama inavyo elekeza, Lakini, Kitabu kipya kimetambulisha masomo mapya kwa Mwaka
B: Somo la 1, Mwanzo 15:1-6; 21:1-3, Wimbo ktk 105:1-9, somo la 2, Ebr
11:8,11-12,17-19 na Injili-Lk 2:22-40. Tafadhali wasiliana na kanisa Mahalia
wameamua nini.)*
-------------------------------------------
KUIGA NJIA ZA FAMILIA TAKATIFU YA NAZARETI
Leo, tunaheshimu familia takatifu ya
Nazaret, Yesu, Maria na Yosefu. Kwa ujumla sisi huwa tuna taswira nzima ya
familia Takatifu. Malaika akimwambia Maria na Yosefu daima pale ambapo kuna
wakati wa hatari na mashaka. Tunaona kama nyumbani kwao Nazareth kuwa kama
sehemu Fulani ya mbinguni ambayo haiingiliwi na mtu, yenye ukamilifu, na sehemu
yenye ukamilifu katika uelewano. Lakini picha hii inatoa mfanano hafifu
kulingana na maisha waliosafiri. Hatuelezwi sana kuhusu maisha ya familia
takatifu katika Injili. Lakini tumepewa kidogo. Tukisaidiwa na hili na hasa
tukisoma kwa undani, tunapata picha tofauti. Tunaona kwamba familia Takatifu
walikumbana na magumu, na katika heshima hiyo tunaweza kusema Kwamba ilikuwa
familia ya kawaida kama yetu.
Wakati ulipo timia kwa Yesu kuzaliwa,
Yosefu na Maria hawakupata sehemu ya kukaa katika vyumba vya wageni. Kuwa na
milango yote ikiwa imefungwa mbele ya macho yako sio kitu cha kujisikia vizuri.
Furaha yao wakati wa kuzaliwa kwa Yesu ilipunguzwa. Hata alipo zaliwa tu
alianza kuwindwa na Herode ili auwawe, na Yosefu na Maria iliwabidi wasafiri
hadi nchi ya ugenini. Kule pia aliweza kufahamu ni jinsi gani ya kuwa mgeni
katika nchi ya watu, kama mkimbizi. Wakati walipo tembelea Yerusalemu, Yesu
aliwapotelea tena, Yosefu na Maria walimtafuta kwa huzuni mioyoni mwao. Wakati
wa maisha yake Maria hakuelewa kila mara alichokuwa akitenda Yesu. Alimuona
akichukuliwa na umati. Na mwishowe kukatokea uchungu wa msalaba, wakati upanga
wa uchungu ulivyo penya moyo wa Maria, na wakati upanga ulivyo penya moyo wa
Mwanae. Familia takatifu haikuwahi kuishi maisha ya uhuru tuu bila kuwa na
misuko suko. Na nikwa jinsi hii tunaweza kuiita familia Takatifu kwasababu
walishinda magumu yote, na ndio maana ni familia ya mfano kwetu.
Familia zetu mara nyingi zinatembelewa pia
na mateso, uchungu, kutokuelewana, tatizo moja au jingine. Maisha yetu mara
nyingine yanatiwa dosari, wakati mwingine yanaanguka kwa pamoja. Hatupaswa
kupatwa na hali ya kukata tamaa na kufa moyo. Familia takatifu inatusaidia
kukuwa katika uimara katika mahusiano yetu. Matatizo na uchungu yanaleta
familia pamoja. Daima tunaitwa na kusamehe, kupenda, na uelewa daima
unakusubiri. Yesu, Maria na Yosefu atusaidie katika kukuwa katika neema kwa
msaada wa Mungu na msaada wa sisi kwa sisi.
Tunaitwa leo kutafakari juu ya umuhimu wa
utume wetu na jukumu la familia ya Kikristo. Familia Baba, Mama na watoto
wanatengeneza familia. Kila mmoja katika familia ana thamani, kupendwa na
kuheshimiwa. Ukamilifu wa maisha ya Familia unaonekana katika familia ya
Nazaret. Katika familia hii tunamuona Yosefu daima akiwa makini katika
kusikiliza sauti ya Mungu, Maria daima akiwa tayari kuyatenda mapenzi ya Mungu
na Yesu daima akiwatii wazazi wake. Ilikuwa ni muunganiko wa watu tofauti. Je, familia
zetu mnaishi kwa umoja wa kijumuiya au mnaishi kwa pamoja kwasababu inalazimu?
Msingi ambao familia inapaswa kujengwa ni
juu ya upendo. Kila mmoja katika familia anapaswa kumchukulia mwenzake kwa
upendo. Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu wanashirikisha upendo
wao na uhai wao kwa viumbe vyote, hasa wanadamu. Yesu alishirikisha upendo huu
kwa familia yake, Maria na Yosefu na wanadamu wote. Je, ni upendo wa namna gani
navuvia katika familia yangu na uzima? Familia ni kanisa la nyumbani. Kitu
muhimu kabisa ambacho familia inapaswa kufanya ni sala katika familia. Kama
tulivyosikia mara nyingi, “Familia inayosali pamoja huishi pamoja”. Inapata
rutuba na vitamin kutoka katika maisha ya sala, je, ninaingia nyumbani kwangu
kama ninavyo ingia kanisani?
Injili ya leo, licha ya Yesu, Maria na
Yosefu, kuna watu wawili ambao ni wazee sana, Simeoni na Anna, ambao walikuwa
wakisali na kumsubiria Masiha katika maisha yao yote. Maadili mengine ya maisha
ya familia ni Wazee, babu na bibi wanaweza kuwafundisha wajukuu, vijana mambo
mema kabisa. Tusiwatenge na kuwaona kana kwamba wamepitwa na wakati.
Sala: Bwana, nisaidie mimi kuishi kama
familia takatifu, tukiungana katika kuheshimiana na upendo. Ninaomba umoja wetu
utupe ujasiri wa kukumbana na changamoto ya maisha. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment