“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano, Desemba 16, 2020,
Juma la 3 la Majilio
Is 45: 6-8, 18-25;
Isa 45: 6-8, 18-25;
Zab 85: 8, 9-13;
Lk 7: 19-23.
JE, NI YESU UNAMSUBIRIA?
Katika Injili ya Luka leo, Yohane
Mbatizaji anawaagiza Wafuasi wamuulize Yesu, “Je, ni yeye ajaye au tumtazamie
mwingine?” Hili pia ni swali la muhimu sana lililopo ndani kabisa mwa moyo wa
kila mmoja wetu, je ni ‘wewe’ ninayekusubiri, ‘ambaye’ nimekusubiri maisha
yangu yote? Na Yesu anakuwa nashauku ya kumjibu Yohane na sisi pia, Yesu anatoa
jibu hili: “Nendeni mkamwambie Yohane mliyo yaona ninyi na kusikia, vipofu
wanapona, viwete wanatembea, wakoma wanaponywa, viziwi wanapata kusikia na
waliokufa wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema”. Kwa maneno mengine,
Yesu anatujibu sisi akisema,”mimi ndiye unayemsubiri, ambaye amekuja kukuokoa
na kufanya mambo yote mapya”
Injili hii inatualika tuyaseme maswali
yetu yaliyo ndani kabisa mwa mioyo yetu, na kwa nguvu kabisa ya unyenyekevu
kama wa Yohane, tumuulize Yesu kilichopo ndani kabisa mwa mioyo yetu. Yesu
anatamani kututimizia hamu ya mioyo yetu, atafanya hivyo tuu kama sisi
tutaonesha unyenyekevu wa kumwomba, kwasababu Yesu haingilii uhuru wa
mwanadamu. Ni jukumu letu tuchague lililo sahihi tutumie uhuru wetu vizuri na
kumwomba yeye, kwani kwa hakika yupo tayari kutimiza tunayotaka kumwomba.
Tunaomba kipindi hiki cha Majilio kiwe
kipindi cha kumtambua Yesu, ukweli, ambao tunautafuta. Tuzamishe mawazo yetu
kwake tuweze kusikia yale yote anayotaka kutuambia Bwana wetu.
Sala: Bwana, nisaidie katika kipindi hiki
cha majilio kuendelea kuandaa moyo wangu. Nisaidie nisikie maneno yako na yote
unayotaka kusema nami. Naomba nikufuate katika yote na kati ya yote nikutambue
wewe kama Mwokozi wa maisha yangu, Mkombozi ambaye nimemsubiria katika maisha
yangu. Yesu, nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment