“MBEGU ZA UZIMA”
Desemba 13, 2020.
------------------------------------------------
DOMINIKA YA 3 YA MAJILIO-DOMINIKA YA
FURAHA
Somo la 1: Isa 61: 1-2, 10-11 Nabii
anadhihirisha kwamba amechaguliwa na Mungu na kutumwa awahubirie maskini habari
njema.
Wimbo wa katikati: Lk 1: 46-48, 49-50,
53-54 Moyo wangu wamtukuza Bwana. Roho yashangilia ukuu wa Bwana wangu, roho
yangu imepata furaha ndani ya Mungu mkombozi wangu.
Somo la 2: 1 Thes 5: 16-24 Paulo
anawaambia Wathesalonike kwamba wasiache kufurahia na kujikabidhi daima katika
kumshukuru Bwana kwa yote aliyowatendea.
Injili: Yn 1: 6-8, 19-28 Yohane
anadhihirisha wazi kwamba yeye sio Masiha. Kazi yake ni ya unyenyekevu
mkubwa-kuandaa njia kwa ajili ya Masiha ambaye tayari yupo katikati ya watu,
ingawaje hawakumtambua.
------------------------------------------------
FURAHI KATIKA BWANA DAIMA
Jumapili ya tatu ya Majilio inajulikana
kama Dominika ya Gaudete au Dominika ya furaha. Hii ni kwasababu Antifona ya
misa, inatualika “tufurahi katika Bwana daima, na tena tufurahi kwasababu Bwana
yupo karibu” (Flp 4:4-5). Neno Gaudete ni neno la kilatini lenye maana
“furahi*. Majilio kuwa kipindi cha kujiandaa kwa ujio wa Masiha (ujio wake kwa
Noeli na ujio wake katika Maisha yajayo), kwa jumapili ya tatu ya majilio tupo
nusu ya kipindi cha majilio, na hivyo kuna haja ya kufurahi tunapoona lengo
letu linakaribia “Bwana yu Karibu”.
Miaka mingi iliyopita mwanafunzi mmoja wa
chuo alikuwa akifanya kazi kama mhasibu, kwenye supermarket moja. Siku moja
akiwa anajaza kumbukumbu katika karatasi. Akawaona wana ndoa wawili wazee
wanaingia ndani huku wakimbeba mtoto mdogo wa kike katika kigari kidogo cha
watoto. Alivyotazama yule mtoto kwa karibu akaona kama ananinginia katika kiti
chake. Akatambua kwamba hana mikono wala miguu na shingo pia. Alikuwa amevaa
kagauni kekundu chenye alama. Wale wana ndoa wazee walivyo msogeza yule mtoto
karibu na yule kijana, yule kijana akampatia yule mtoto kitu Fulani cha
kuchezea. Yule kijana akapokea hela kutoka kwa wale wazee, lakini huku akiinua
kichwa na kumtazama yule mtoto, yule mtoto hakuacha kumchekea kwa furaha kubwa
sana ambayo hajawahi kuiona. Gafla huyu kijana alivutwa na jinsi huyu mtoto
alivyo vutwa naye na kujikuta anamtazama kwa akili zake zote. Huyu mtoto
alimtoa kutoka katika hali ya kutokuwa na furaha hasa akiwaza maisha ya chuoni
na kumleta katika ulimwengu wa furaha, ulimwengu wake wa furaha, upendo na
kujali. Kwa kuwasha mshumaa wa tatu wa Majilio, tunaitwa na kukumbushwa kwamba
tunaitwa tufurahi zaidi katika ulimwengu wetu wa mateso na uchungu.
Katika kitabu chake, “Muache Mungu
akubariki” John Killinger alimalizia kwa changamoto: Mruhusu Mungu akubariki.
Usijitazame na kuangalia jinsi maisha yalivyo magumu. Tazama huko na huko uweze
kuona jinsi maisha yalivyojazwa na fumbo na uzuri ndani yake. Tazama ni kwa
jinsi ghani ulimwengu unapendeza. Tazama jinsi ulimwengu unavyopendeza wakati
unajua Mungu yupo kazini akiukomboa na kuwaondoa wale wanao uharibu, ili
ubinadamu na utakatifu na huruma na kiu ya kutaka haki na Amani ijazwe na thamwabu
iwepo katika maisha ya milele. Mpe Mungu shukrani kwa zawadi ya uwepo wake.
Alafu tazama huku na huko uangalie utaweza kumshirikisha nani. Na ambaye
atakufanya tajiri wa furaha ya Kimungu.
Kama utatamani kuishi hivi kila siku,
utakuwa na jambo ndani ya moyo wako kabla huja kaa pamoja katika mstari wa
wafuasi. Furaha itatiririka ndani ya moyo wako kama mto na utalala kitandani
mwako usiku kwa furaha. Na utasema, “Litukuzwe jina la Mungu wetu milele na
milele, anayetuita daima katika sheria mpya ambapo wenye haki watakuwa wakiimba
daima”.
Isaya, anamtabiri Yesu katika somo la
kwanza “ametumwa na Bwana ili alete faraja kwa maskini kuwaponya waliovunjika
moyo, kutangaza uhuru kwa wafungwa”. Unaweza kuwa mfungwa wa dhambi,
uliyevunjika moyo kwasababu ya marafiki wabaya, mfungwa katika eneo lako la
kazi au kwenye ndoa. Unaweza kufanywa mnyonge na kuwa chini kwasababu ya hali
ambayo ipo nje ya uwezo wako. Mruhusu Yesu aingie katika maisha yako; muache
yeye achukue nafasi juu ya tatizo lako. Jikabidhi katika muongozo wake
nasikiliza sauti yake. Somo la pili kutoka barua kwa Wathesalonike linarudia
nakusema, “anayewaita ninyi ni mwaminifu, na kwamba atakamilisha”. Hupaswi kuwa
mpweke. Utakuwa mpweke pale tu utakapo amua kujitenga mwenyewe kutoka kwa
Mungu.
Furaha ni nini? Ina majibu mengi, lakini
furaha kamili ni kule kuwa na uhakika kwamba upo na Mungu na Mungu mwenyewe
ndiye anayeongoza maisha yako. “Kwa Mungu wangu ipo furaha ya moyo wangu” Isaya
anasema, “kwani amenivika vazi la ukombozi”. Furaha pia inaelezwa kama hali ya
moyo na akili ambayo inakuja kwasababu ya kukutana na ndugu zetu, kufungua
mioyo yetu kwao, kuwa sehemu ya mateso yao na fuaha yao. Tunapata furaha kwa
yale ambayo tunawapimia wenzetu na kuwashirikisha. Lakini pengine furaha kubwa
ni ile hali ya kusamehe, hali ya kusamehe na kusamehewa. Ndio maana furaha
kubwa imeshikwa na Mungu, ambaye ndiye anaye jenga na kuunda msamaha wenyewe.
Tunaweza kufuharia furaha ya Kimungu pale tunapo wasamehe wengine, sio mara
moja tu lakini daima na daima. Kuna furaha moja tunaweza kuwa nayo ambayo tuna
hakika nayo, nayo ni kusamehewa na Mungu..na wale tulio wakosea.
Kwa kipindi hichi cha majilio tufanye
maamuzi ya kweli ya kumruhusu Mungu atubariki atupe matumaini mapya na
kutuwekea hali mpya ya kuishi. Tuishi tukiwa na maana kwamba giza la wakati huu
sio lengo letu la mwisho la maisha yetu, yapo mengi yanayokuja. Katika njia hii
tutaanza kupata furaha kama mto ndani yetu, kama ile ya Bikira Maria, Yosefu,
wachungaji na wafalme.
Sala: Bwana Yesu, ninakusubiri kwa makini
nikisubiri kupokea uponyaji wako na uhuru. Yesu tusaidie tukurudie, tunaomba
tuone uso wako na tujazwe na furaha. Yesu, nakutumaini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment