“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Alhamisi,
Novemba 12, 2020,
Juma
la 32 la Mwaka wa Kanisa
.
Flm1:7-20;
Zab
145:7-10;
Lk
17:20-25
UFALME
WA MUNGU UPO KATI YETU.
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana
linaanza kwa kuiangalia zaburi yetu ya wimbo wa katikati ambapo tunakutana na
maneno yasemayo ana heri yule anayesaidiwa na Bwana. Bwana asipokusaidia
kusonga mbele itakuwa tabu sana. Tunakuwa kama wale waliokuwa wanajenga mnara
wa Babeli-badala ya kujenga walibomoa au wana Wamisri walipokuwa wanawakimbiza
waisraeli ndani ya ile bahari-mambo yalienda kinyume chao. Bwana akienda
kinyume nasi tutakwama katika mengi-tutalima hatutavuna, tutavuna na kushindwa
kula-kama ilivyotokea kwa yule tajiri mpumbavu, na tutakula pasipokuwa na afya
kama inavyojitokeza kwa baadhi yetu kila siku.
Wengi
tumevuna mali tukashindwa hata kuila, na wale tunaoila hata hatupati afya-ni
matatizo kila siku. Mambo kama haya yanatukumbusha tumrudie Mungu na kumtegemea
zaidi.
Katika
somo la kwanza, Honesmo ndiye anayeonyesha kusaidiwa na Bwana. Yeye kabla ya
kujiunga na ukristo, alikuwa mtumwa aliyemilikiwa na mwingine lakini baada ya
kuingia ukristo-ukristo unamrudishia utu wake na Paulo anachukua muda
kumwelezea Bwana wa huyu Honesmo kwamba ampokee kama mtoto wake kama ambavyo
angempokea yeye. Huu ndio ukuu wa imani yetu kwa Kristo. Kwa kweli ni ya
thamani kubwa. Tuitunze vyema imani hii.
Na
pia tuwaone wenzetu hata kama ni maskini kuwa watu wenye hadhi. Kwa njia ya
imani yao katika Kristo, wamepewa utu. Tutumie utu huu vyema. Tusinyanyase
yeyote.
Somo
la injili linazungumzia juu ya ujio wa ufalme wa Mungu. Anasisitizia kwamba
ufalme wa mbinguni upo katikati yao. Hapa alimaanisha zaidi kwamba ufalme huu
unapaswa uwe moyoni mwao.
Mioyo
yetu iutangaze ufalme huu kwa kile kinachotoka ndani yake, kwa maneno
tunayosema na kinywa chetu, mawazo yetu na matendo. Wengi bado tunatangaza
ufalme wa shetani kutokana na picha tunazotuma, miziki tunayosikiliza, filamu
tunazoangalia na muda tunaotumia katika kuangalia picha mbaya ndani ya simu
zetu. Vitu vya Mungu hatuvipatii muda, hata ile siku ya Jumapili bado
inaonekana kama siku ya starehe na anasa kuliko kusali. Dhambi nyingi
zinatendeka ndani ya siku hii ya jumapili kuliko siku nyingine. Tuombe
kutangaza utawala huu kwa umakini zaidi.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment