MASOMO YA MISA, NOVEMBA 12, 2020
SOMO
1
Flm.
7 – 20
Nalikuwa
na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu
imeburudishwa nawe, ndugu yangu.
Kwa
hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasako; lakini, kwa
ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paulo mzee, na sasa mfungwa
wa Kristo Yesu pia. Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika vifungo
vyangu, yaani, Onesimo; ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana,
wewe na mimi pia; niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moy wangu hasa;
ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo
vya Injili.
Lakini
sikutaka kutenda neno lolote isipokuwa kwa shauri lako, ili kwamba wema wako
usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari. Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe
kwa muda, ili uwe naye tena milele; tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya
mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili
na katika Bwana. Basi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama
mimi mwenyewe. Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike ndicho juu
yangu. Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii
kwamba nakuwia hata nafsi yako. Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika
Bwana; uniburudishe moyo wangu katika Kristo
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
146:7 – 10 (K) 5
(K)
Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Bwana
huishika kweli milele,
Huwafanyia
hukumu walioonewa,
Huwapa
wenye njaa chakula,
Hufungua
waliofungwa. (K)
Bwana
huwafumbua macho walopofuka,
Bwana
huwainua walioinama,
Bwana
huwapenda wenye haki,
Huwahifadhi
wageni. (K)
Huwategemeza
yatima na mjane,
Bali
njia ya wasio haki huipotosha.
Bwana
atamiliki milele,
Mungu
wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi.
Aleluya.
(K)
SHANGILIO
Zab.
27:11
Aleluya,
aleluya,
Ee
Bwana, uifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
INJILI
Lk.
17:20-25
Yesu
alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia,
Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au,
kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
Akawaambia
wanafunzi, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku moja katika siku zake Mwana
wa Adamu, msiione. Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke
mahali mlipo, wala msiwafuate; kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande
huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana
wa Adamu katika siku yake. Lakini kwanza, hana budi kupata mateso mengi, na
kukataliwa na kizazi hiki.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment