“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi,
Novemba 26, 2020,
Juma
la 34 la Mwaka wa Kanisa
Ufu
18:1-2, 21-23; 19:1-3, 9;
Zab
99:2-5;
Lk
21:20-28
UAMINIFU
WA MUNGU!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana
katika somo la kwanza Yohane anaeleza juu ya kuteketea kwa yule kahaba mkuu,
aliyewahi kuwa maarufu na kujiona kutawala dunia nzima. Anaaibishwa na kibao
kinawageukia wale aliowatesa; wakati wanaanza kufurahia utawala wa Mwenyezi
Mungu, yeye atakaa katika shida.
Somo
hili linatoa somo kwetu sisi hasa sisi tunaonekana na baadhi ya watu kuwa ni
vijana, maarufu, wababe, wenye misuli na waheshimiwa. Heshima hizi au ujana
wetu au misuli yetu hazitasalia nasi kwa miaka yote. Upo wakati nasi tutakuwa
wazee, watoto tuliowanyanyasa watakuwa na nguvu zaidi yetu na kila
tutakapotamani kuwa na nguvu kama zamani, kamwe hatutafanikiwa tena. Hivyo
duniani tuishi kipole. Tusimnyanyase yeyote hata akiwa maskini, mtoto au
kichaa. Nyakati zinabadilika pia.
Kati
yetu kuna waliowahi kuwa maarufu sana, tukaponda ujana kweli lakini kwa sasa
hivi tumechakaa kabisa na tunashindwa kuamini kwamba upo wakati tuliowahi kuwa
vijana na sisi. Tuishi kipole, tutumie misuli yetu, ujana wetu, usichana wetu
vyema na tumtukuze nao Mungu. Haya yote yana mwisho.
Katika
injili Yesu anaendeleza tena juu ya ukweli kwamba mambo ya dunia yana mwisho
kwa kueleza juu ya shida atakazopata Yesusalemu. Huu ulikuwa mji maarufu,
ulijiona kufahamu mengi, kuwa na viongozi hodari, kuwa na hekalu la Mungu, kuwa
na makaburi ya wakuu kama Daudi. Walifikiri mji huu hautakaa ushindwe.
Lakini
mwishowe walijishangaa kuona ukianguka na wengi kuuangamia. Haya yatatokea na
kwetu endapo tutaishia kujisifia na kujitangaza kuwa watakatifu bila ya sisi
kufanya bidii kila siku. Anayejitangazatangaza kwamba yeye ni mteule wa Bwana
na kujidai kwamba atalindwa tu na Mungu bila ya kuongeza bidii na kumwomba kila
siku ulinzi huanguka kihivihivi na kukamatwa na shetani.
Shetani
huwakamata kirahisi walio na majivuno; wanaojiita kwamba wameokoka na kumbe bado
wapo katika udhaifu na hawakazani kumwomba Mungu awaokoe. Sisi tupunguze
majivuno na kumwomba Mungu kama hitaji letu na hapa tutaweza kumpokea Mungu
siku ya Mwisho na yeye kutuokoa.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment