MASOMO YA MISA, NOVEMBA 26, 2020
ALHAMISI,
JUMA LA 34 LA MWAKA
SOMO
1
Ufu.
18:1 – 2, 21 – 23; 19:1 – 3, 9
Mimi,
Yohane, naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu;
na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka,
umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho
mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.
Na
malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa
katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule
mkuu, wal ahautaonekana tena kabisa. Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga
zomari, nay a wapiga filimbi, nay a wapiga baragumu, haitasikiwa ndani yako
tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yoyote hataonekana ndani yako tena
kabisa; wal asauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wal
anuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana arusi na
bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako
walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
Baada
ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni,
ikisema, Aleluya; Wokovu na utukufu na nguvu zina Bwana mungu wetu; kwa kuwa
hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu
aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake
mkononi mwake. Wakasema mara ya pili, Aleluya. Na moshi wake hupaa juu hata
milele na milele.
Naye
akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwanakondoo.
Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
100 (K) Ufu. 19:9
(K)
Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwanakondoo.
Mfanyieni
Bwana shangwe, dunia yote,
Mtumikieni
Bwana kwa furaha;
Njoni
mbele zake kwa kuimba. (K)
Jueni
kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye
aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu
watu wake, na kondoo wa malisho yake. (K)
Ingieni
malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani
mwake kwa kusifu;
Mshukuruni,
lihimidini jina lake. (K)
Kwa
kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema
zake ni za milele;
Na
uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)
SHANGILIO
Zab.
25:4, 5
Aleluya,
aleluya,
Ee
Bwana, unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:20-28
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na
majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Ndipo walio katika
Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio
katika mashamba wasiuingie. Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapitilizo, ili
yatimizwe yote yaliyoandikwa. Ole wao wenye miamba na wanaonyonyesha katika
siku hizo!
Kwa
kuwa kutakuwa na shida katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. Wataanguka kwa
ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na
Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.
Tena,
kutakuwa na ishara katika jua; na mwenye, na nyota; na katika nchi dhiki ya
mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu wakivunjika
mioyo kwa hofu, na kwa kutazama mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu z
ambinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika
wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Basi mambo hayo yaanzapo kutokea,
changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment