“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Alhamisi,
Novemba 5, 2020
Juma
la 31 la Mwaka
Flp.
3:3 – 8
Zab.
105:2 – 7 (K) 3
Lk.
15:1-10
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo tafakari yetu
inaongozwa na maneno ya zaburi yetu ya wimbo wa katikati kwamba enyi mumtafuato
Bwana mioyo yenu ifurahi; wajivunie jina na matendo ya Bwana.
Furaha
ya namna hii ni dhihirisho la roho iliyotulia, inayoridhika, isiyo na tamaa,
imetoshekwa na kile Bwana alichotoa na hivyo basi inakuwa na kila sababu ya
kufurahi. Furaha na kuridhika na utulivu ni viashirio vya roho iliyobarikiwa na
Bwana.
Paulo
katika somo la kwanza anaonesha kuridhika na imani yake na neema Kristo alizomjalia
kiasi cha kuwa tayari kutangaza wema huu. Kama asingalikuwa na furaha na
kuridhika katika imani yake mpya hakika asingaliweza kuwashawishi Wafilipi
wajiunge naye. Nasi lazima tuonyeshe furaha na kuridhika katika imani yetu na
Ukristo wetu.
Tuwe
na furaha, furaha ni ushuhuda unaowavutia wengine kuja kwa Kristo. Furaha
inamvuta mwingine. Sisi tukiwa watu wa huzuni na kulalamika katika maisha huwa
tunawakwaza wengine kumfuata na kumwamini Mungu.
Katika
injili, Yesu anaeleza kwamba amekuja kuwatafuta waliopotea. Anakiri kwamba
mbele ya Mungu wanadamu wote wanahadhi sawa na wanapendwa kabisa. Hata wale
wanaokataa upendo huo bado anazidi kuwatafuta ili basi awaokoe na wanapokubali
kweli kunakuwa na furaha kubwa sana.
Somo
hili limguse kila mmoja wetu leo. Pale tunapoungama na kukataa dhambi ama kweli
ni furaha kubwa kwa Yesu. Sisi tunaoishi uasherati, kuishi uchumba sugu-pale
tutakapoamua kufunga ndoa na kuacha dhambi hizo ama kweli itakuwa ni furaha
kubwa sana mbele ya Mungu. Leo tuache vilema vya dhambi leo. Pia tuwe
wavumilivu zaidi katika kuwatafuta waliopotea-unaposhindwa kumrudisha
aliyemdhambi kundini na kumwacha aangamie-jua kwamba ni kushindwa mtihani na
hapa tunakuwa tumeshindwa vibaya zaidi. Sisi tusiwe watu wa kukata tamaa kwa
haraka na tuzidishe bidii katika kuwavuta wenzetu waliopotea.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment