MASOMO YA MISA, NOVEMBA 5, 2020
SOMO
1
Flp.
3:3 – 8
Sisi
tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala
hatuutumaini mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu yeyote
akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nalitahiriwa siku
ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa
Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi,
mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na
hatia. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa
ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa
ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
105:2 – 7 (K) 3
(K)
Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
Mwimbieni,
mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini
ajabu zake zote.
Jisifuni
kwa jina lake takatifu,
Na
ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. (K)
Mtakeni
Bwana na nguvu zake,
Utafuteni
uso wake sikuzote.
Zikumbukeni
ajabu zake alizozifanya,
Miujiza
yake na hukumu za kinywa chake. (K)
Enyi
wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake,
Enyi
wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye
Bwana, ndiye Mungu wetu,
Duniani
mwote mna hukumu zake. (K)
SHANGILIO
Yn.
10:27
Aleluya,
aleluya,
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
INJILI
Lk.
15:1-10
Watoza
ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia Yesu wamsikilize. Mafarisayo
na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi,
tena hula nao. Akawaambia mfano huu, akisema, Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia,
akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aenda
akamtafute yule aliyepotea hata amwone? Naye akiisha kumwona, humweka mabegani
pake akifurahi. Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake,
akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu
aliyepotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya
mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda
ambao hawana haja ya kutubu.
Au
kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na
kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? Na akiisha kuiona, huwaita
rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa
nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha
mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment