“MBEGU ZA UZIMA”
Tafakari ya kila Jumapili
Jumapili, Novemba 8, 2020.
Juma la 32 la Mwaka
Hek 6:12-16;
Zab 62:2-8;
1 Thes 4:13-18;
Mt 25: 1-13
TAA ZINAZO WAKA
Somo la kwanza linaimba
sifa za hekima. Wakati huo huo linasema kwamba hekima inaweza kupatikana na
wale wanayo itafuta. Katika somo la pili
Paulo anawafariji watu wa Wathesalonike ambao wana wasiwasi na wapendwa wao
ambao walishafariki. Anawaambia kwamba hakika Mungu atawafufufa kama alivyo mfufua Mwanaye Yesu Kristo.
Katika somo la Injili Yesu anatuambia tuwe tayari kwani hatujui siku wala saa.
Katika hali ya kwanza
kabisa mfano huu unaonekana hautendi haki. Unaonekana sio sawa kwasababu hawa
wanawali watano hawakaribishwi katika harusi kwasababu tu, taa zao zimeisha
mafuta. Lakini ukweli ni kwamba huu mfano unaenda ndani zaidi ya hilo. Kuna
kitu zaidi ya taa za mafuta. tunaweza kuuelezea katika hali ya kisasa kwa namna
ifuatayo.
Wale wanawali ni kama
wanawake kumi walioenda kwenye duka kununua kitu kwa ajili ya Noeli. Wakaondoka
mapema wakiwa na shauku kubwa, sehemu zilizo salama karibu na saloni ya nyewele
mjini. Kila mmoja amebeba begi na kulishika vizuri ili asije mtu kumpokonya. Wanawake
watano walikuwa na hekima na wakarimu. Walikuwa ni watu wafanyakazi wazuri sana
ambao wameshafanya sadaka sana kwa ajili ya kuhifadhi kwa ajili ya
kununua. Walitaka kupata punguzo kubwa
angalao kwani kila mmoja alikuwa na familia ya kutunza. Walikuwa hawafikirii
sanaa juu yao wenyewe bali pia watoto wao na nyumbani kwao. Wengine watano
walikuwa ni wajinga na wapumbavu. Hawakuwa na hali ya kuhifadhi kidogo kwa
ajili ya nyumbani na watoto. walikuwa wakifikiria tu mambo yao wenyewe.
Stoo ile ya kuhifadhi
vitu ilichelewa kufunguliwa. Kusubiri kwao walichoka sanaa. Wanawake wote kumi
walilala. Gafla kukasikika sauti. Stoo ilikuwa ikifunguliwa na kila mtu
akafanya bidii kuwahi. Hapo ndipo wale wapumbavu walipotambua kuwa wana hela
kidogo kwenye pochi zao. Walisahau kwamba wiki iliopita walienda kununua vitu
na wakatumia hela nyingi sana kwa ajili yao wenyewe. Katika kuchanganyikiwa
wakawarudia wale wenye hekima kuwaomba wawape hela kidogo , tutawapa tukifika
nyumbani, wakasema samahani tuna kidogo tu kwa ajili yetu wenyewe. Huu ndio muda wetu tunaweza kukimbia nyumbani
mara moja na kirudi, wakiwa wanasema hivi, wale wenye busara wakaenda ndani. Na
wale wajinga wakabaki pale njee. Wakachukuwa teksi mara moja kwenda nyumbani.
Lakini muda waliofika nakwenda benki wakarudi wakakuta tayari stoo ipo tupu.
Mwenye stoo akawaambia samahani sina cha kufanya ni makosa yenu. Kwanini
hamkuja kwa wakati? Wakatambua kwamba alikuwa akiwahoji sawa, wakaondoka wakiwa
wamechanganyikiwa na bila furaha, kwasababu ya uzembe wao.
Na sasa turudi kwenye
mfano wa Yesu. Kwa wale wanawali wenye busara ilikuwa ni muda tuliopewa wakuishi.
Ni kitu ambacho walikiishi na kuthamini na kujiandaa. Hali hii haikuwa ni ya
kujirudia ili kukutana na Bwana harusi na kuingia karamuni. Hakukuwa na njia
yeyote yakuikosa. Kwa wanawali wasio na busara ni tofauti. Wao walichukulia
kuwa ni kitu cha kawaida, na kufanya kwa mazoea. Na hivyo wakashindwa kuingia
ndani. Lakini ukweli ni kwamba ni mfumo wa maisha yao yote ulikuwa mbaya. Kwa
njia nyingine hawakuhukumiwa kwasababu ya kosa moja la maisha yao. Wale wenye busara walikuwa tayari na makini,
walikuwa wakiyatenda yote yaliosemwa. Wale watano wengine hawakuwa tayari na
wala hawakuwa wamejiandaa, walikuwa wasikilizaji wa maneno tu bila kutenda.
Kwetu sisi somo
linaonekana dhahiri. Sisi hatujishughulishi na stoo. kwamba. Ni maisha yetu ya
umilele yalio hatarini. Kuna hatari ya kujikuta sisi wenyewe tumefungiwa njee
katika karamu ya mwisho. Wakati sauti ya Bwana itakavyo sikika. Yote ambayo
atahitaji hatataka kujua ni mtu wa namna ghani, wala sio mimi ni mangapi nilio
nayo. Je, itakuwaje tukikamatwa tukiwa hatuja jiandaa? Tunapaswa kukuta daima
taa zetu zinawaka. Tunapaswa kuweka mafuta daima. Bwana anaweza kuja wakati
wowote.
Lakini tusisahau kwamba
tunaalikwa kwenye sherehe ya maana sana. Ni kwenye harusi sio mazishi. Ni
furaha sana kwamba wote tuna mwaliko. Kama tumemfanya Yesu ni rafiki katika
barabara yetu, ni wazi kwamba siku hiyo haitatukuta bila kujitambua au
kujiandaa.
Tunaitwa kushikilia na
kubeba mwanga wa Kristo. Lakini ni wazi kama wale wanawali wapumbavu kuna
wakati na sisi tunakosa mafuta kwasababu ya kutojishugulisha kwetu mara
nyingine. Na kuruhusu taa hii kupungukiwa na mafuta. Kwa njia ya sala na kuwa
tayari, Yesu atatusaidia kuhakikisha taa zetu zinabaki zikiwa zinawaka.
Sala: Bwana tusaidie
tuweze kuweka mwanga wa taa ya imani yako ukiwa unawaka daima. Tunaomba
tusishikilie kitu kingine zaidi, na kwa kufanya hivyo tuweze kukutana nawe kila
unapotuita. Yesu, nakuamini wewe. Amina
-------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment