MASOMO YA MISA, NOVEMBA 8,
2020
DOMINIKA YA 32 YA MWAKA
MWANZO:
Zab. 88:2
Maombi yangu yafike mbele
zako, uutegee ukulele wangu sikio lako, Ee Bwana.
_____________
SOMO 1
Hek. 6:12-16
Hekima hung’aa, wala
hafifii;
Huonekana upesi nao
wampendao;
Hupatikana nao
wamtafutao.
Hutangulia kujionyesha
kwao wamtakao,
Amtafutaye mapema hana
kazi ngumu;
Atamkuta ameketi mlangoni
pake.
Kumtia fikirani ni
ufahamu mkamilifu;
Naye mwenye kukesha kwa
ajili yake
Atakuwa mara hana
masumbufu.
Yeye huzunguka-zunguka
mwenyewe,
Akiwatafuta wao
wanaomstahili;
Njiani hujidhihirisha
kwao kwa upendo,
Hukutana nao katika kila
kusudi.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 63:1-7 (K) 1
(K) Ee Mungu, Mungu
wangu, nafsi yangu inakuonea kiu.
Ee Mungu, Mungu wangu
nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea
kiu.
Mwili wangu wakuonea
shauku,
Katika nchi kama na
uchovu, isiyo na maji. (K)
Ndivyo nilivyokutazama
katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na
utukufu wako.
Maana fadhili zako ni
njema kuliko uhai,
Midomo yangu itakusifu.
(K)
Ndivyo nitakavyokubariki
maadamu ni hai,
Kwa jina lako nitainua
mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai kama
kushiba mafuta na vinono,
Kinywa changu kitakusifu
kwa midomo ya furaha. (K)
Ninapokukumbuka kitandani
mwangu,
Nakutafakari Wewe makesha
yote ya usiku.
Maana Wewe umekuwa msaada
wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako
nitashangilia. (K)
_____________
SOMO 2
1Thes. 4:13-18
Ndugu, hatutaki msijue
habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na
matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo
na hao waliolala katika yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twaambieni
haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja
kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu
Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika
mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili
tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi,
farijianeni kwa maneno hayo.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
_____________
SHANGILIO
Yn. 14:23
Aleluya, aleluya,
Mtu akinipenda atalishika
neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake.
Aleluya.
_____________
INJILI
Mt. 25:1-13
Yesu aliwaambia wanafunzi
wake: Ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao,
wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano
wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta
pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na
taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini
usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi, tokeni mwende kumlaki.
Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazingeneza taa zo. Wale wapumbavu
wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na
ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Na hao waliokuwa
wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye
arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema,
Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment