“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatano,
Novemba 11, 2020.
Juma
la 32 la Mwaka
Tit
3:1-7;
Zab
23
Lk
17: 11-19.
SHUKRANI!
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu asubuhi ya leo katika adhimisho la
Misa Takatifu. Leo katika zaburi yetu ya wimbo wa katikati, tunakutana na Daudi
akitoa ushuhuda wa jinsi Mungu alivyomchungaji mwema kwa wale wanaomba ulinzi
kwake. Yeye mwenyewe aliomba ulinzi huu na kuupata kwa kuwa maisha yake
yalijawa na misukosuko ya kutafutwa auawe.
Ndivyo
ilivyo hata kwa nyakati zetu. Labda baadhi yetu tunaishi katika ujirani mgumu
kiasi kwamba wanaokuzunguka wanataka hata nafsi yako iangamie lakini ni kwa
sababu tu hawana uwezo wa kufanya hivyo. Hata ukiwa na hakika na ukweli kuna
baadhi ya watakaokuchukia. Katika mazingira ya namna hii hatuna jinsi isipokuwa
kujikabidhi mikononi mwa Mungu na kuomba ulinzi kama alivyofanya Daudi. Na
silaha kuu itakayotuokoa hasa katika lile eneo tunapochukiwa na wenzetu ni
kuishi maisha mema yasiyo na 'scandals', dhambi au kulipiza kisasi. Maisha mema
ndiyo yatakayotufanya tuwashinde maadui wa namna hii.
Ndiyo
Paulo anayomsisitizia Tito kuyasisitizia katika somo la kwanza. Kipindi hiki
wakristo walikumbwa na maadui wengi na kilichowaokoa ni sala na maadili yao
mema. Sisi tutambue kwamba maisha mema yasiyolipiza kisasi ni silaha ya
kumshinda adui. Mara nyingi tunashindwa na maadui kwa sababu wanatukamatia
kirahisi katika uovu au 'scandals' zetu na hapa wanatufunga mdomo. Tuishi
maisha mema iwe silaha yetu katika Bwana.
Kwenye
somo la injili Yesu anafurahishwa na kitendo cha mkoma Msamaria kuja na kutoa
shukrani. Wasamaria hawakuelewana vizuri na Wayahudi. Yesu kama Myahudi
anamtendea wema mkuu bila ya kujali uhusiano wao wa kiasili na hili tendo jema
linamfunga mdomo huyu Msamaria na anadiriki kuja na kujitupa miguuni mwa
Myahudi kushukuru.
Sisi
tusiache kuwafanyia 'surprise' maadui zetu kwa kuwatendea mambo mema hata kama
wao wanatutendea mabaya au kutuwazia mabaya. Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment