MASOMO YA MISA, NOVEMBA 11, 2020
JUMATANO,
JUMA LA 32 LA MWAKA
SOMO
1
Tit.
3:1-7
Uwakumbushe
watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila
kazi njema; wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha
upole wote kwa watu wote. Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili,
tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi,
tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
Lakini
wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa,
ulituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema
yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; ili
tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele,
kama lilivyo tumaini letu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
23 (K) 1
(K)
Bwana ndiye mchungaji wangu.
Bwana
ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa
na kitu.
Katika
malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando
ya maji ya utulivu huniongoza.
Huniuisha
nafsi yangu. (K)
Huniongoza
katika njia za haki kwa ajili ya jina lake,
Naam,
nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa
mabaya,
Kwa
maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo
lako na fimbo yako vyanifariji. (K)
Waandaa
meza mbele yangu,
Machoni
pa watesi wangu.
Umenipaka
mafuta kichwani pangu,
Na
kikombe changu kinafurika. (K)
Hakika
wema na fadhili zitanifuata,
Siku
zote za maisha yangu;
Nami
nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)
SHANGILIO
Zab.
19:11-19
Aleluya,
aleluya,
Amri
ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
INJILI
Lk.
17:11-19
Ikawa
walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa akipita katikati ya Samaria
na Galilaya. Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye
ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa,
uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa
walipokuwa wakienda walitakasika.
Na
mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti
kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je!
Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka,
enenda zako, Imani yako imekuokoa.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment