“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
tafakari
ya kila siku
Jumamosi,
Novemba 21, 2020,
Juma
la 33 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu
ya kutolewa Bikira Maria Hekaluni
Zek 2:14-17;
Lk
1:46-55;
Mt
12:46-50
SADAKA
ILIYO KAMILI!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo tunaadhimisha
sikukuu ya kutolewa Bikira Maria hekaluni. Ni siku inayoonesha kwamba Bikira
Maria alikuwa chombo kiteule cha Mungu, kilichoandaliwa na Mungu tangu kuzaliwa
kwake na wazazi wake walikuwa wacha Mungu waliomuandaa vizuri kiroho.
Kwa
desturi za kabila la Israeli na kuendana na sheria ya Mungu, sheria ilikuwa ya
kuwatolea watoto hekaluni iliwahusu wanaume walio vifungua mimba tu-wanawake
hawakulazimika kisheria. Kitendo cha Maria kutolewa hekaluni chaonesha kwamba
wazazi wake walifanya mpaka ziada, walifanya zaidi ya kile cha sheria na hii
kwa kweli ilionesha umuhimu wa Bikira Maria kama chombo kiteule cha Mungu. Hii
ndiyo kumbukumbu yetu ya leo ilivyo na masomo yetu ya leo yanatusaidia vizuri
kutafakari kumbukumbu hii.
Somo
la kwanza kutoka katika kitabu cha nabii Zekaria. Hapa tunaona Mungu akionesha
kupitia kwa nabii Zekaria kwamba Israeli ni chombo kiteule cha Mungu kilichochaguliwa
na Mungu kwa kazi yake maalumu. Hivyo anaahidi kuwatetea, kupambana na mataifa
yaliyowatesa na lengo la kufanya hivi ni kumfanya Israeli awe mfano kwa mataifa
mengine-yaani mataifa mengine yakitaka kumjua Mungu wa kweli waende Israeli,
wakitaka kuona litrujia safi waende Israeli, wakitaka kuona uongozi mzuri
waende Israeli; hivyo, lengo lilikuwa ni wote waone, waache uovu na wamgeukie
Mungu wa kweli.
Hapa
tunaona kwamba japokuwa Israeli alikuwa chombo kiteule cha Mungu, alikuwa na
wajibu wa kutimiza pia; alipaswa kuhakikisha anashika sheria ya Mungu na
kuepuka kuwakwaza wengine, ili awe mfano kwa wengine katika kumjua Mungu.
Yesu
anapigilia msumari suala hili kwa kusema kwamba heri yule anayelisikia neno la
Mungu na kulishika; huyo ana heri kwani kwa maisha yake atawaongoza wengi kwa
Mungu; atamfanya Mungu atukuzwe na wengi.
Kinachosemwa
katika haya masomo ndicho kilichotokea kwa Maria. Yeye alikuwa chombo kiteule
cha Mungu na kwa sababu hiyo aliamua kutokumwangusha Mungu. Alihakikisha anaishika
kweli sheria ya Mungu na ndio sababu za kutolewa hekaluni lengo ni kuishi
sheria ya Mungu.
Ndugu
zangu, kwa utii wa huyu Mama, dunia ilipata ukombozi, dunia iliokolewa kutoka
katika dhambi ya asili na sasa tuna mkombozi wetu Yesu Kristo. Shukrani sana
kwa utii wa Bikira Maria, shukrani sana kwa wazazi wake.
Ndugu
zangu, kwetu sisi, Wakristo sherehe hiii ina ujumbe mzito kwetu. Kwa ubatizo
wetu nasi tumetolewa hekaluni. Tunapaswa kutambua hili. Hivyo, ishi kanuni za
Kristo. Jua kwamba ukiishi ukristo wako vyema, unawafanya wengi wamtukuze
Mungu, unakuwa chanzo cha wengi kuja kwa Mungu, unasaidia utawala wa Kristo
uendelee Zaidi. Lakini ukiishi bila kufuata mashauri ya Kristo, unamsaidia
shetani kuendeleza mamlaka yake, unakuwa mjumbe, balozi wake, yaani
unamdidimiza Kristo na shetani anaanza kutawala.
Hivyo,
muonee Kristo huruma jamani. Ameshakuja na kufa hapa duniani. Mateso yote yale
aliyompata na bado unazidi kumtumia shetani kama mvuvio wako? Niambie shetani
alishawahi kumwaga hata tone moja la damu yake ili akuokoe? Niambie ndugu
yangu. Hivyo, jua kwamba ukikataa kuishi maisha ya Kikristo vizuri, ukiwa
unaendelea kutenda dhambi, ukiwa unatazama mapicha mapicha kwenye simu yako
tena ya ajabu ajabu-jua kwamba unasaidia utawala wa shetani kukua.
Hivyo,
siku ya leo tutafakari sheria zetu na tuziishi, tusimwachie mwanya shetani.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment