Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, NOVEMBA 21, 2020

 

MASOMO YA MISA, NOVEMBA 21, 2020

JUMAMOSI, JUMA LA 33 LA MWAKA

 

KUMBUKUMBU YA KUTOLEWA BIKIRA MARIA HEKALUNI

 

SOMO 1

Zek. 2:10-13

 

Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa, kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile,, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako. Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena. Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.

 

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

 

WIMBO WA KATIKATI

Lk. 1:46-55 (K) 46

 

(K) Mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu.

 

Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

Na roho yangu imemfurahia Mungu,

Mwokozi wangu. (K)

 

Kwa kuwa ameutazama,

Unyonge wa mjakazi wake.

Kwa maana, tazama, tokea sasa

Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;

Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,

Na jina lake ni takatifu. (K)

 

Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi

Kwa hao wanaomcha.

Amefanya nguvu kwa mkono wake;

Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao. (K)

 

Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi;

Na wanyonge amewakweza.

Wenye njaa amewashibisha mema,

Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. (K)

 

Amemsaidia Israeli, mtumishi wake;

Ili kukumbuka rehema zake;

Kama alivyowaambia baba zetu,

Ibrahimu na uzao wake hata milele. (K)

 

SHANGILIO

Lk. 1:28

 

Aleluya, aleluya,

Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Umebarikiwa katika wanawake.

Aleluya.

 

INJILI

Lk. 11:27 – 28

 

Yesu alipokisema maeno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.

 

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.

 

-------------------------

Copyright © 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

 

No comments:

Post a Comment