“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Novemba 16, 2020,
Juma
la 33 la Mwaka wa Kanisa
Ufu.
1:1 – 4; 2:1 – 5
Zab.
1:1 – 4, 6 (K) Ufu. 2:7
Lk.
18:35-43
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Naomba tafakari yetu
iongozwe na maneno ya wimbo wa katikati kwamba yule ashindaye atampatia nafasi
ya kula katika mti wa uzima.
Kiitikio
hiki kinatualika kubakia imara hadi mwisho kwani vishawishi ni vingi na
anayetunzwa ni yule tu anayebakia kuwa imara hadi mwisho. Wengi huwa tunaanza
vyema lakini shida ni kudumu hadi mwisho.
Zaburi
hii inatumika kutusaidia katika kulitafakari somo la kwanza hasa kwa ule ujumbe
wa kanisa la Efeso. Kanisa hili lilianza vyema kiimani tangu Paulo alipohubiri
huko Injili. Walikataa falsafa za kipagani na kuwapinga baadhi ya wale wakristo
ambao walirubuniwa na mafundisho ya uongo na kuingiza falsafa katika mafundisho
ya Kristo na mwishowe wakaishia kuupoteza ukristo kabisa.
Kanisa
hili lilikuwa hodari. Lakini kidogokidogo lilianza kulegea na ufunuo wa Yesu
leo unaliambia likazane zaidi liongeze bidii. Ndio ujumbe ambao Yesu anataka
kutuambia kila mmoja wetu siku ya leo. Yabidi nasi kuwa watu wa bidii zaidi,
mara nyingi ile siku ya kufunga ndoa au kupata upadre au nadhiri au komunio au
kipaimara huwa tunakuwa motomoto sana. Lakini tunaanza kupungua taratibu. Sasa
ni lazima tuzidishe bidii kila wakati; huu ndio ukristo wenyewe.
Mara
nyingi tunaanguka kwa sababu ya uzembe na kupunguza bidii. Sisi tuzidishe bidii
yetu zaidi. Hii ndio itakayotuokoa. Kama nipo kazini nizidishe upendo na
kuongea na wenzagu vizuri zaidi. Kama ni daktari niongeze bidii na kuacha
uzembe wa kuhudumia. Nisikubali kupoteza uhai wa mtu kwa uzembe wangu.
Katika
somo la injili, tunakutana na kipofu mmoja aliye na bidii kumwamini na kumfuata
Yesu. Yeye anapokatazwa na wenzake asije kwa Yesu, moja kwa moja anaongeza
bidii, anazishinda kelele za wale wanaomzuia na mwishowe anamfikia Yesu na
kupata uponyaji. Sisi tuzidishe bidii ya kumtumikia Yesu. Tusitishwe na maneno
ya wenzetu pembeni watakaokasirika kwa kitendo cha wewe kuacha ulevi au kuacha
urafiki mbaya nao. Njia hii ndio itakayokufanya umfikie Yesu na kupata toka
kwake uponyaji na kuokolewa.
Wengi
tumeshindwa kubadilika kwa sababu tunatishwa sana na kelele za wenzetu walioko
karibu yetu ati wanasema nini. Wakisema vibaya tu juu yetu tunaacha kile kizuri
tunachofanya na kwenda kuwafuata. Hapana. Tusiishi namna hii. Tubadilike. Tuwe
watu wapya wakumsikiliza Mungu anataka nini, tusiogopeshwe na maneno ya watu.
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment