MASOMO
YA MISA, NOVEMBA 16, 2020
JUMATATU,
JUMA LA 33 LA MWAKA
SOMO
1
Ufu.
1:1 – 4; 2:1 – 5
Ufunuo
wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba
hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa
wake Yohane: aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani,
mambo yote aliyoyaona. Heri asomaye na wao wayasikiao yoe aliyoyaona. Heri
asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa
humo; kwa maana wakati u karibu.
Yohane,
kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia: Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo
kwake yeye aliyeko na laiyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba
walioko mbele ya kiti chake cha enzi.
Nilisikia
Bwana ananiambia: Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo
anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye
aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu
yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena
umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa
na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakin nina neno
juu yako, nay a kwamba umeuach aupendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi
ulioanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
1:1 – 4, 6 (K) Ufu. 2:7
(K)
Yeye ashindaye, nitampa matunda ya mti wa uzima.
Heri
mtu yule asiyekwenda,
Katika
shauri la wasio haki;
Wala
hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala
hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Bali
sheria ya Bwana ndiyo impendezayo,
Na
sheria yake huitafakari mchana na usiku. (K)
Naye
atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando
ya vijito vya maji,
Uzaao
matunda yake kwa majira yake,
Wala
jani lake halinyauki;
Na
kila alitendalo litafanikiwa. (K)
Sivyo
walivyo wasio haki;
Nao
ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
Kwa
hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,
Wala
wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. (K)
SHANGILIO
Mt.
4:4
Aleluya,
aleluya,
Mtu
hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
18:35-43
Yesu
alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba
sadaka; na alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, Kuna nini? Wakamwambia,
Yesu wa Nazareti anapita. Akapiga kelele, akisema, Yesu Mwana wa Daudi,
unirehemu. Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi
sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu.
Yesu
akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza, Wataka
nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona. Yesu akamwambia, Upewe kuona;
Imani yako imekuponya. Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza
Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment