“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Takari
ya kila siku
Jumanne,
Novemba 10, 2020,
Juma
la 32 la Mwaka wa Kanisa
Tit
2:1-8, 11-14;
Zab
36:3-4, 18, 23, 27, 29;
Lk
17:7-10
MTUMISHI
MWAMINIFU!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu. Leo katika zaburi yetu ya wimbo wa
katikati tunakutana na maneno kwamba Bwana huwapatia wokovu wote wamchao. Hivyo
zaburi hii inawatia moyo wale wamtumainiao Bwana waendelee kumtegemea na wale
wasiomtegemea Bwana wazidishe bidii. Ni mwaliko kwamba kila mmoja wetu awekeze
kwa Bwana kwani Bwana haachi kumpatia wokovu yeyote awekezaye kwake.
Zaburi
hii inatumika kutilia mkazo ujumbe wa Paulo kwa mfuasi wake Tito. Kipindi hiki
Paulo alijiona kufikia mwisho wa utume wake na hivyo alimtegemea zaidi Tito.
Tito alipaswa kuonesha mfano na kuwasisitiza watu kufundisha kwa njia ya mfano
wao wa kimaisha. Kina mama wenye umri wanaalikwa kuwa mfano kwa kina mama
wadogo; mfano wa utii hasa kwa waume zao. Na kinababa wenye umri wanapaswa kuwa
mfano kwa waliowachanga hasa katika suala la tamaa kwamba wasiwe watu wa tamaa.
Somo
hili linamgusa kila mmoja wetu kwa siku ya leo. Linatueleza kwamba umri ni
lazima uendane na hekima pia. Lakini kuna kati yetu ambao kadiri umri
unavyoongezeka, ndivyo hekima yetu inapungua. Hapa yabidi kumuomba Mwenyezi
Mungu ili hekima yetu iongezeke. Tunapozeeka bila hekima yetu kuongezeka ni
aibu kubwa kwa upande wetu kwani tunaangaliwa na wengi. Tuone uchungu
tunapokutwa tukipigana vikumbo au kubishana pengine na wajukuu wetu
tukigombania vitu vya kijinga tu. Tuombe Mungu atufanye hekima yetu iongezeke kadiri
ya umri wetu pia.
Injili
ya leo inatufundisha tunganganie utumishi. Utumishi ni hekima tosha ambayo
inatupasa ikue pamoja nasi kadiri umri unavyoongezeka. Hii inatusaidia kuishi
na wengi ndani ya dunia hii na kuepuka makwazo mengi. Mara nyingi sisi tulio na
umri tunagombana na wale wadogo kwa sababu mara nyingi tunataka wao
watutegemeze na kututumikia. Lakini tutakapogeuza mtazamo ili nasi
tuwategemeze-hakika tutaishi nao katika amani kubwa.
Tuombe
kuishi utumishi. Hii ndio hekima inayopaswa kukua nasi kadiri ya umri wetu
unavyoongezeka maishani. Namna hii tutakuwa mfano.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment