MASOMO YA MISA, NOVEMBA 10, 2020
SOMO
1
Tit.
2:1–8, 11–14
Wewe
nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu,
wenye busara, wazima katika Imani na katika upendo na katika saburi. Vivyo
hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji,
wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake
vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye
kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao
wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
Vivyo
hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; katika mambo yote ukijionyesha wewe
mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyehsa
usahii na ustahivu, na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makossa, ili
yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
Maana
neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa
ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katiak
ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye Baraka na mafunuo ya utukufu
wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa
ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake
mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
37:3–4, 18, 23, 27, 29 (K) 39
(K)
Wokovu wa wenye haki una Bwana.
Umtumaini
Bwana ukatende mema,
Ukae
katika nchi, upendezwe na uaminifu.
Nawe
utajifurahisha kwa Bwana,
Naye
atakupa haja za moyo wako. (K)
Bwana
anazijua siku za wakamilifu,
Na
urithi wao utakuwa wa milele.
Hatua
za mtu zaimarishwa na Bwana,
Naye
aipenda njia yake. (K)
Jiepue
na uovu, utende mema,
Na
kukaa hata milele.
Wenye
haki watairithi nchi,
Nao
watakaa humo milele. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:18
Aleluya,
aleluya,
Unifumbue
macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
Aleluya.
INJILI
Lk.
17: 1-10
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au auchungaye
ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule
chakula? Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie,
hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? Je! Atampa asante
yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? Vivyo hivyo nayi, mtakapokwisha
kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya
tu yaliyotupasa kufanya.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment