MASOMO YA MISA, NOVEMBA 7, 2020
SOMO
1
Flp
4:10 – 19
Nalifurahi
sana katika Bwana, kwa kuwa sas mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili
yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifiriri hali yangu; lakini hamkupata nafasi. Si
kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali
yoyote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yoyote,
na katika mambo yoyote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na
kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye atiaye nguvu. Lakini mlifanya
vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu.
Nanyi
pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi ya kuwa katika mwanzo wa Injili,
nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa linguine lililoshirikiana nami katika
habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. Kwa kuwa hata huko
Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. Si kwamba
nakitamani kile kipawa bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi katika
hesabu yenu. Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea
kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka
yenye kibali, impendezayo Mungu. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji
kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. Sasa atukuzwe
Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
ZAB.
112:1 – 5 (K) 1
(K)
Heri mtu yule amchaye Bwana.
Aleluya,
Heri
mtu yule amchaye Bwana,
Apendezwaye
sana na maagizo yake,
Wazao
wake watakuwa hodari duniani,
Kizazi
cha wenye adili kitabarikiwa. (K)
Heri
atendaye fadhili na kukopesha,
Atengenezaye
mambo yake kwa haki.
Kwa
maana hataondoshwa kamwe,
Mwenye
haki atakumbukwa milele. (K)
Moyo
wake umethibitika hataogopa,
Amekirimu,
na kuwapa maskini,
Haki
yake yakaa milele,
Pembe
yake itatukuzwa kwa utukufu. (K)
SHANGILIO
Yn.
13:13
Aleluya,
aleluya,
Bwana
anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote
niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
16:9-15
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana
wawakaribishe katika makao ya milele. Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana,
huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo,
huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Bali, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika
mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Na kama hamkuwa
waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?
Hakuna
mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu au
kumpenda huyu, ama atamshikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia
Mungu na mali.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment