“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi
Tafakari ya kila siku
Jumanne,
Novemba 7, 2020
Juma
la 31 la Mwaka
Flp
4:10 – 19
ZAB.
112:1 – 5 (K) 1
Lk.
16:9-15
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu asubuhi ya leo katika adhimisho la
Misa Takatifu. Leo tafakari yetu inaanza kwa kuiangalia zaburi yetu ya wimbo wa
katikati inayosisitizia heri kwa yeyote amchaye Mwenyezi Mungu. Huyu atatulia
kabisa, na kuwa na moyo thabiti. Hatayumbishwa na vitu kama njaa, ukosefu wa
fedha, elimu au cheo. Yeye moyo wake utatulia kwa Bwana.
Moyo
wa namna hii ndio aliokuwa nao Paulo katika somo la kwanza. Yeye alimtegemea
Mungu na hivyo basi haogopeshwi na misukosuko yote ya ulimwengu huu. Hashtushwi
na njaa au kushiba, utajiri au umaskini, kuwa navyo au kutindikiwa.
Amekwishajifunza kuvumilia hali zote. Ukiona tunayumbishwa na mambo kama haya,
basi tutambue kwamba hatumchi Mungu. Kweli kukubali kukosa usingizi au kupata
pressure ati kwa sababu nimekosa Pesa ya kunywa bia au nimekataliwa na msichana
au kijana amenikataa-au wenzangu wamependelewa kuliko mimi ni dalili za
kutokumcha Mungu.
Mungu
hutuwezesha kuyaweza mambo yote. Tunapokubali kushindwa na vidogo hivi ni lazima
tujiulize-je?-kweli ninamtegemea na kumcha Mungu, kwa nini nipewe pressure na
kitu hiki? Tumtegemee Mungu tupate kuzishinda hali za namna hii.
Katika
injili Yesu anasema kwamba hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili-mara nyingi
ukitumikia mali na Mungu kwa wakati mmoja, kinachotokea ni kumnyima Mungu
nafasi. Unaifanya ile mbegu iliyooteshwa isongwe na miiba ya ulimwengu na
itashindwa kuzaa. Wengi wetu hata siku ya jumapili hatuendi kanisani ili
tufanye biashara. Ukweli ni kwamba ukianza kwa kutumikia mali, utamtupa Mungu
pembeni tu na utamkosa. Lakini ukianza kwa kumtumikia Mungu utapata yote.
Tupambane
na uchoyo, tumpatie Mungu haki yake, ili basi tupate kubarikiwa naye. Tumtolee
sadaka bora kama Abeli. Tuache kumtolea vile vitu vya mwisho au chenchi au zile
pesa zilizotoboka na kuchanika. Tumpe Mungu kile kilichobora kukiri ukuu wake.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment