MASOMO
YA MISA NOVEMBA 3, 2020
JUMANNE,
JUMA LA 31 LA MWAKA
SOMO
1
Flp.
2:5-11
Iweni
na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye
yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu
kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa
namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama
mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Kwa
hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani,
na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa
utukufu wa Mungu Baba.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
22:25-31 (K) 25
(K)
Kwako zinatoka sifa zangu, Ee Bwana.
Nitaziondoa
nadhiri zangu
Mbele
yao wamchao.
Wapole
watakula na kushiba,
Wamtafutao
Bwana watamsifu;
Mioyo
yenu na iishi milele. (K)
Miisho
yote ya dunia itakumbuka,
Na
watu watamrejea Bwana;
Jamaa
zote za mataifa watamsujudia.
Maana
ufalme una Bwana,
Naye
ndiye awatawalaye mataifa.
Wakwasi
wote wa dunia watakula na kusujudu. (K)
Wazao
wake watamtumikia.
Zitasimuliwa
habari za Bwana,
Kwa
kizazi kitakachokuja,
Nao
watawahubiri watakaozaliwa haki yake,
Ya
kwamba ndiye aliyeyafanya. (K)
SHANGILIO
Mt.
4:4
Aleluya,
aleluya,
Mtu
hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
14:15-24
Mmojawapo
wa wale walioketi chakulani pamoja na Yesu alimwambia, Heri yule atakayekula
mkate katika ufalme wa Mungu. Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa,
akaalika watu wengi, akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale
walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. Wakaanza
wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti
niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe
jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimeoa
mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.
Yule
mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye
nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu
na vichochoro vya miji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na
viwete. Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, n ahata sasa
ingaliko nafasi.
Bwana
akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe
kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. Maana nawaambia ya kwamba katika wale
walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment