“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne,
Novemba 3, 2020
Juma
la 31 la Mwaka
Flp
2: 5-11;
Zab
22: 25-31;
Lk
14: 15-24.
MAJUKUMU
YA KIKRISTO!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Mungu
katika zaburi yetu ya katikati, kwenye shairi la kwanza tunakutana na maneno
yasemayo kwamba maskini watakula na kushiba. Hawa wanakula si kwa sababu ya
kuwa na uwezo au pesa za kuwashibisha bali hali yao ya kinyenyekevu na udogo na
utayari wao ndio utakaowafanya washibe.
Dhana
ya utayari katika somo la kwanza tunaona ikimfanya Yesu akwezwe juu kuliko
vyote-utayari wa kukubali kufa msalabani ambako kwa Wayahudi ilikuwa ni
kulaaniwa lakini akawa tayari kuchukua laana na kweli akapata ukuu.
Wale
wanaoalikwa katika karama na huyu aliyeandaa karama katika injili walikosa ule
utayari na kukazania yao na ndio wakaishia kukosa mwaliko mkuu. Maskini
walikuwa na utayari wa kwenda na kufaidi.
Nasi
ndugu zangu tukikosa utayari tutaishia kutokushiriki karamu kama hawa waliokuwa
wamealikwa. Wengi wetu tumeshindwa kutumiwa na Mungu kwa sababu ya kukosa
utayari. Na wengi tumekosa neema nyingi kwa Mungu. Hata baadhi yetu tukifaulu
kidogo darasani tunaishia kusema siwezi kujiunga na utawa-nimefaulu mno, nataka
niwe daktari. Hapa ni namna mojawapo ya kukosa utayari. Au pale baadhi tunasema
kama nina uwezo, sitaki kusoma masomo ya dini, nataka nisome 'secular'-hapa
kweli ni kukosa utayari.
Hata
kanisani wale wenye uwezo tunakataa kuhudhuria misa jumapili na kuwaachia
maskini waende kanisani na sisi tunaendelea na biashara hadi jumapili. Hapa ni
kukosa utayari. tungekuwa na utayari hakika tungebarikiwa zaidi.
Mungu
hufanya kazi na wale walioko tayari. Maskini wako tayari wakati wowote kwa
sababu hawana cha kushikamana nacho. Walio na mali wanakosa utayari, kila kitu
wanaona ugumu kujitoa kwa Mungu; kumpatia Mungu muda fulani bado wanaona shida.
Tutambue
kwamba pale tunapoanza kuwa wachoyo kwa Mungu ndio mwanzo wa kuanguka. Hawa
walioalikwa wamekuwa wachoyo na kukosa ukarimu na utayari kwa ndugu zao na huu
ndio ukawa mwanzo wao wa kuanguka. Sisi tubadilike. Tuwe na utayari. Utayari
utatufanya tuchanue zaidi.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment