MASOMO YA MISA, NOVEMBA 24, 2020
JUMANNE,
JUMA LA 34 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
1
Ufu.
14:14 – 19
Mimi,
Yohane, niliona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja,
mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono
wake mundu mkali. Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa
sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune;
kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa. Na yeye
aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa.
Kisha
malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana
mundu mkali. Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye
mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali,
akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana
zabibu zake zimeiva sansa. Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi,
akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la
ghadhabu ya Mungu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
96:10 – 13 (K) 13
(K)
Bwana atauhukumu ulimwengu kwa haki.
Semeni
katika mataifa, Bwana ametamalaki;
Naam,
ulimwengu umethibitika usitikisike,
Atawahukumu
watu kwa adili.
Mbingu
na zifurahi, nchi na ishangilie,
Bahari
na ivume na vyote viijazavyo. (K)
Mashamba
na yashangilie, na vyote vilivyomo,
Ndipo
miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha;
Mbele
za Bwana, kwa maana anakuja,
Kwa
maana anakuja aihukumu nchi.
Atauhukumu
ulimwengu kwa haki,
Na
mataifa kwa uaminifu wake. (K)
SHANGILIO
Yak.
1:21
Aleluya,
aleluya,
Pokeeni
kwa upole neno la Mungu, lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:5-11
Watu
wa kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa
kwa mawe mazuri na sadaka za watu, Yesu alisema, Haya mnayoyatazama, siku
zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Wakamwuliza
wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo
hayo ya karibu kutukia?
Akasema,
Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu,
wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao. Nanyi
mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi
kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi. Kisha aliwaambia, Taifa
litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na
matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha
na ishara kuu kutoka mbinguni.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment