MASOMO
YA MISA, NOVEMBA 22, 2020
DOMINIKA
YA 34 YA MWAKA A
SHEREHE
YA BWANA WETU YESU KRISTU MFALME
MWANZO:
Ufu.
5:12; 1:6
Astahili
Mwana-Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na
heshima. Utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele.
SOMO
1
Eze.
34:11-12, 15-17
Bwana
Mungu asema hivi; Tazama mimi mwenyewe, naam, mimi, nitawatafuta kondoo zangu,
na kuwaulizia. Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo zake, siku ile anapokuwa
kati ya kondoo zake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo zangu; nami
nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.
Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu, nami nitawalaza, asema Bwana Mungu.
Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudihsa waliofukuzwa, nitawafunga
waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu;
nitawalisha hukumu. Na kwa habari zenu, Enyi kundi langu, Bwana Mungu asema
hivi; Tazama, nahukumu kati ya mnyama na mnyama, kondoo waume na mbuzi waume
pia.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
23;1-3, 5-6 (K)
(K)
Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Bwana
ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa
na kitu,
Katika
malisho ya majani mabichi hunilaza. (K)
Kando
ya maji ya utulivu huniongoza;
Huniuisha
nafsi yangu, na kuniongoza,
Katika
njia za haki kwa ajili ya jina lake. (K)
Waandaa
meza mbele yangu,
Machoni
pa watesi wangu.
Umenipaka
mafuta kichwani pangu,
Na
kikombe changu kinafurika.
Hakika
wema na fadhili zitanifuata,
Siku
zote za maisha yangu.
Nami
nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)
SOMO
2
1Kor.
15:20-26, 28
Kristo
amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na
mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu
wote wanakufa, kadhalika katika Kristo wote watahuishwa. Lakini kila mmoja
mahali pake, limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. Hapo
ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote,
na mamlaka yote, na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake
wot echini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. Basi, vitu
vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini
yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Mk.
11:10
Aleluya,
aleluya,
Abarikiwe
Yeye ajaye kwa jina la Bwana: Ubarikiwe na Ufalme ujao, wa Baba yetu Daudi.
Aleluya.
INJILI
Mt.
25:31-46
Hapo
atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote
pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote
watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo
na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa
na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa
maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa
mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja
kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu,
wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu
tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi,
tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na
Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa
hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale
walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto
wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na
njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni,
msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije
kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe
una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni,
tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea
mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao
kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa
milele.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment